
Roma Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show
maalum ya Washindi wa Kili Music Award jijini
Mbeya katika Uwanja wa Sokoine jana.

Suma Lee nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta
raha kwa mashabiki katika wakati wa show
maalum ya Washindi wa Kili Music jijini Mbeya

Ben Paul nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuletya
raha kwa mashabiki katika wakati wa show maalum
ya Washindi wa Kili Music Award jijini Mbeya.

Barnaba Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji
Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo wakati wa
show maalum ya Washindi wa Kili Music Awards
jijini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine

Vijana wengi walikuwa wamepigilia vitu vya namna hii

Mashabiki walikuwa hawatulii

Mkali wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba jukwaani
hii wakati wa show maalum ya Washindi wa
Kili Music Award iliyofanyika uwanja wa Sokoine

Wasichana waliokuwa wakitoa huduma ya tiketi

Mkali wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba na Omy Dimpoz
katika wimbo Nai Nai akiimba jukwaani hii wakati
wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award
iliyofanyika uwanja wa Sokoine

Dimpoz akipitika katikati ya wacheza show wake.


Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani
na wacheza sho wake wakati wa show maalum ya
Washindi wa Kili Music Award jijini Mbeya

Back Stage mambo yalikuwa hivi, Toka kushoto ni
Ali Kiba, Omy Dimpoz, Ben Pol na Meneja wa
Omy Dimpoz Mubenga.
HABARI KWA HISANI YA FAZA KIDEVU BLOGSPOT
MANENO
ya Injili yanayosema Wamwisho anakuwa wakwanza na wakwanza akawa
wamwisho yametima hii leo katika Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya pale
mkali wa Hip Hop, Roma Mkatoliki alipoongoza jahazi la wakali wa Tuzo
za Kili Musc Award 2012 katika onesho lao la Uwanjka wa Sokoine mjini
Mbeya jana.
Roma
akipanda juukwaani akisindikizwa na DJ maarufu DJ Choka, alishangiliwa
vilivyo na umati wa watu uliofurika uwanjani hapo pale tu ilipofika zamu
yake kupanda jukwaani.
Roma!
Roma! Roma! Roma!....hayo ndio yalikuwa maneno ya shwangwe kutoka kwa
wapenzi wa burudani kutoka Jijini Mbeya waliofurika katika Uwanja wa
Sokonine mjini hapa kushuhudia show hiyo kali ya Washindi wa Tuzo za
Kili Music Award 2012.
Roma
baada ya kumaliza kuimba nyimbo zake kaza aliwashukuru wana Mbeya kwa
kura zao zilizompa ushindi na kuwaambia sasa anamaliza show hiyo ambayo
hadi hapo alipofikia alisema wametumia Sh 200/= pekee kati ya Sh 2,000
ya kiingilia waliyotoa.
“Sasa
ndugu zangu, nawaambia ukweli hadi sasa mmesha tumia sh 200 tu ya
kiingilio chezu,..sasa nawapa show ya Sh 1,800 iliyobaki,” alijigamba
Roma ambaye muda wote alikuwa akishangilia na ndipo alipomaliza kwa
kuimba Wimbo wa Mathematic uliompa tuzo.
Wasanii
wengine waliopanda jukwaani hii leo ni pamoja na Ben Pol, AT, Ali Kiba ,
Barnaba, Omy Dimpoz na Suma Lee nao wamefunika vibaya katika Tamasha
la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika katika Uwanja wa sokoine
Mjini Mbeya.
Alianza jukwaani kupanda mshindi wa Tuzo ya wimbo Bora wa R&B.
Msanii
Ben Paul ambaye alijinyakulia tuzo hiyo kupitia kibao Number One ambapo
nae alishambulia jukwaa na kuwaamsha watu kuwa sasa show imeanza.
Alifuata
jukwaani Suma Lee ambaye aliongozwa na show kali kutoka kwa vijana wake
wane wakike na wakiume na kushangiliwa vilivyo kwa mkongwe huyo wa
Bongo Fleva.
Baada
ya Ben Pol, alipanda mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo
Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT na kutoa burudani ya nguvu na
wimbo wa Vifuu Utundu amabao ulimpa tuzo aliucheza vilivyo na
wanenguaji wake wawili wa kike.
Ika
fika zamu ya Omy Dimpoz jukwaani kwa kuimba nyimbo yake mpya aambayo
alitaraji kuizindua jana katika Ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es
Salaam, single ya Baadae kasha ile iliyo mpa tuzo ya Wimbo bora wa
Kushirikishwa ya Nai Nai aliyo anza kuimba pekeyake na baade kuurudia
wimbo huo akiwa na Ali Kiba.
Ali
Kiba alibaki jukwaani hapo kama ilivyokuwa mjini Moshi na vijana wake
kumfuata kutoa shukrani zao za kupata kura zilizo wapa ushindi wa tuzo
ya Wimbo bora wa Zouk Rhumba kupitia wimbo wa Dushelele.
Wakati
mara zote pazia la utoaji burudani kwa washindi hao wa tuzo za Kili
Music Award 2012 wanaofanya ziara limekuwa likifunga na Roma Mkatoliki
leo akapnda wapili kutoka mwisho.
Roma
ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo
wake wa Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia
jukwaa huku viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka na hata alipomaliza
show yake bado mashabiki walimtaka aendelee.
Mshindi
wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa Kiume, Barnaba ndiye aliyefunga pazia hilo
kwa siku ya leo mjini Mbeya kwa kuimba ikiwapo inayovuma kwa sasa ya
Magube Gube.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment