October 26, 2014


 Mwongozaji wa kipindi cha wanawake live cha EA TV joyce Kirya amefunguka kuhusu watanzania na miss Tanzania

soma hapa
Watz saluti kwa kushika mabango.....ila ninamaswali machache...
Ivi Miss Tanzania ina faida gani kwa Maisha ya Watanzania Masikini wenye Taifa Tajiri ambalo hata rais wake hajui ni kwanini wananchi wake ni masikini???
Ivi umejaribu kufikiri Miss Tanzania inasaidiaje Kuboresha maisha yako na ya watanzania masikini walio wengi tena walioko vijijini???
Miss tz inaboreshaje huduma za Afya ili kupunguza vifo vya wanawake, watoto na watanzania masikini wenye nchi Tajiri???
Miss tz inaboreshaje Elimu nchini hasa shule za Umma ambazo wengi wanaosoma huko ni watoto wetu sisi watanzania masikini wenye Tanzania Iliyojaa Utajiri????
Miss Tz inaboreshaje huduma ya maji nchini wakina mama wengi tunabakwa kwa kufuata maji umbali mrefu???
Hii nguvu inayotumika kwa miss tz, kwa nini tusiihamishie kwenye mustabakali wa maisha yetu ya sasa na ya baadae yaani vizazi vijavyo kwenye Katiba pendekezwa???
"Katiba pendekezwa" umewahi kuifuatilia hata kwa dk 1??? Unajua kama ndo imebeba maisha yako, wajukuu wako, vitukuu na vilebwe??? Una mchango gani katika kupata Katiba Bora ya nchi yetu! umeshajiuliza na kutafakari???
Tuache kutumia fikra zetu kwenye vitu visivyo vya msingi katika maisha ya watanzania tulio wengi.... samahani lakini
Miss tz fanya yako mama...pole kwa yalokukuta.. waandaaji Wamekupa taji wenyewe kwa sababu zao wenyewe, so wasikusumbue..tena wakuache kabisa Mwanamkelive wangu, ningekuwa mimi ni wewe nisingeenda kwenye press ya kujichoresha...dhambi hii abebe Mratibu wa mashindando na team yake...
Watz tulio wengi ni Wajinga sanaaa hasa katika kuchekecha masuala yapi ya Msingi na yapi ya yasiyo ya Muhimu! na si kosa letu bali ni mikakati ya watawala wetu kuhakikisha wananchi tunajikita kuongelea Mambo ambayo hayana Msingi sana kwa wananchi wengi, badala ya kufuatilia masuala ya msingi yanayohusu hatma zetu... na wamefaulu katika hilo na wataendelea kufaulu kwa sababu ubora wa Elimu yetu inazidi kuporomoka...usitegemee mtz aanze kuongelea mfano uchakachuaji wa Katiba Pendekezwa, wala kuhoji huduma muhimu zinazotokana na kodi yake.. never!!!
Mfano rahisi angalia kwenye mitandao ya kijamii ya watanzania na ulinganishe na nchi zingine mambo wanayoyapa kipaumbele katika kuyajadili kwa nguvu kama hii tuliyoweka kwa Miss Tz...Ukilinganisha Nguvu inayotumika kwenye Katiba Pendekezwa na Nguvu ya Miss Tz kuna tofauti kubwa sana...
Pia Angalia magazeti yanayosomwa sana, kisha utawajua watz tulio wengi.. si wote.. utatujua tuliowengi ni watu wa aina gani....
Waandishi wenzangu watendeeni Haki watanzania masikini ambao Taifa lao ni Taifa Tajiri sana lakini ndo Taifa lenye watu masikini sana...waandishi ndo maana tunaitwa makanjanja!! Ivi kweli airtime na rasilimali kubwa hivi mkaziweka kwa nguvu yote hii in the name of Miss Tz???? Ebu tuwahurumie Watz na sisi wenyewe na Taifa letu hili..... sisemi kama msiandike ila mmeshupalia sana kana kwamba Miss Tz ni "Katiba pendekezwa"
Natamani sana waandishi wenzangu, nguvu hiyo mngeniuliza mimi Joyce Kiria ni yapi nimeyaona huku mkoa wa Mara Wilaya ya Tarime ambapo nimekuja kufanya kazi zangu kama kawaida za kumkomboa Mwanamke na mtoto wa Tanzania...
Majibu yangu yangekuwa hivi:
> Mkoa wa Mara umebarikiwa fursa mbalimbali kama Madini, Bandari Kavu na Ardhi yenye rutuba ambayo inapata mvua za kutosha na wanalima mara mbili kwa mwaka...

> Jamii ya watu wa Mara ni watu wenye kuheshimu sana watu pamoja na mila na desturi zao, ni watu wakarimu sana, ni watu wachapa kazi sana...
> Kwenye hii jamii ya watu wa Mara huwezi kukuta watoto wa mitaani! Si kwa sababu hakuna watoto yatima bali kwa sababu ya Thamani ya Utu wameiweka kwa MTU... kwa hiyo watoto waliofiwa na ndugu zao wanalelewa na jamaa zao...
> Baadhi ya Changamoto ...
Ukeketaji ndo changamoto kubwa sana huku.. ikifuatiwa na nyumba Ntobu, (wanawake wanaolewa na wanawake wenzao) yapo mengi sana ila naachia hapa kwa sasa...Ningewaeleza kwa undani.. buhahahahaha

Kiukweli Binafsi ninauchukia Ujinga kwa namna yeyote ile..... historia ya kutokusoma kwangu si sababu ya mimi kuukumbatia Ujinga...Ujinga naulinganisha na Umasikini, na ndo maana nafanya kazi kwa bidii! kwangu mimi Ujinga ni pale ambapo mtu Hujui kitu na Hutaki kujua Ukweli wa jambo au masuala fulani... kuwa mjinga si dhambi lakini usipofanya bidii ya kuuondoa Ujinga Hujitendei Haki hata wewe mwenyewe.. Samahani lakini kama nimekukwaza.....ni mtazamo tu usijenge chuki au vipi??? Buhahahahaaa

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE