Shilole na Nuh Mziwanda
Mziwanda akijiandaa kumvisha pete ya uchumba mkewe mtarajiwa Shilole
Staa wa kibao cha Chuna Buzi, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amevishwa pete ya uchumba na mumewe mtarajiwa  ‘Nuhu Mziwanda’ wakati alipokuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa hapo jana(Dec.20)   iliyofanyika Mikocheni jijini Dar es salaam.
Hafla hiyo ndogo  ilihudhuriwa na mastaa kidhaa akiwemo aliyekuwa Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere, Shetta, Martin kadinda, Millard Ayo pamoja na jamaa wa karibu wa wapendanao hao ambao walikuwa mashuhuda wa tukio zima la kuvishana pete.
Shilole na Mziwanda1
 Shishi baby akionyesha pete ya uchumba aliyovishwa

Mziwanda na Shilole
Baada ya tendo zima la kuvishana pete, kilichofuata kilikuwa ni kukata keki ya birthday aliyoandaliwa Shilole katika siku yake hiyo maalum

Shilole akifungua shampeni
shilole akifungua Champagne

Mziwanda akizungumzia juu ya ujio wa ngoma yake mpya zimataa
Mtangazaji wa Clouds fm, Millard Ayo akimhoji Mziwanda