May 29, 2016

alikiba1

Baada ya kuachia wimbo wa ‘Aje’ kumbe wasanii waliotajwa kwenye wimbo huo walikuwa hawajui kwa mujibu wa Alikiba.Wimbo wa ‘Aje’ hauna muda mrefu tangu Alikiba ameuachia lakini umezidi kufanya vizuri kwenye TV na Radio huku kwenye mtandao wa Youtube video yake ikiwa imeshatazamwa zaidi ya mara laki nane.

Akiongea kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Alikiba alisema, “Wenyewe walikuwa hawajui kuwa nimewaimba.”
“Wema nilimwambia siku moja kuwa bichwa nina suprise yako, ila Lulu sikuwahi kumwambia na hata sijui ameipokeaje, ila naamini kaipokea fresh,” aliongeza.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE