June 30, 2016

DSC_8618
Mtangazaji wa kipindi cha ‘Mboni Show’, Mboni Masimba Jumatano hii kwenye viwanja vya Karimjee alifuturisha watoto yatima kutoka kwenye vituo vitano vya mkoa wa Dar es Salaam.
Futari hiyo ilihudhuriwa na Makamu wa Rais, Samiah Hassan Suluhu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mufti mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Salum, Mabalozi wa nchi mbalimbali, watu maarufu pamoja na wageni wengine waalikwa.
Akihutubia mara baada ya futari hiyo, Mboni alieleza kuwa, wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara hii ni kutokana na kurudisha fadhila kwa jamii kwa kidogo kinachopatikana hivyo amewaomba wadau wengine kujitokeza kufanya jambo kama hilo kila inapohitajika kwa jamii.
Aidha Mama Samia alimpongeza Mboni kwa tukio hilo kuwa ni la kuigwa hivyo ni lazima jamii imuunge mkono kwa kujilea kwake.

Mboni
“Nakupongeza Mboni na timu yako kwa kuwakumbuka watoto hawa. Tukio kama hili kuliandaa linahitaji gharama na kujitolea haswa. Tupo pamoja nawe na juhudi zako tunaziona nakupongeza sana,” alisema Mama Samia.
Aidha, Mama Samia Suluhu amesema serikali inaendelea kuvisimamia kwa ukaribu vituo vyote vya kulelea watoto yatima nchini na vituo ambavyo vitabainika kuwa vinanufaisha wamiliki na vinaendeshwa bila ubora vitafungiwa mara moja.
Makamu wa Rais amesema kuwa azma ya serikali ni kuona vituo vyote vya kulelea watoto yatima kote nchini vinatoa huduma bora na inayokidhi mahitaji ya watoto hao na sio vinginevyo.

DSC_8611
Kuhusu malezi ya Watoto yatima, Makamu wa Rais ametoa wito kwa jamii iendelee kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwapatia elimu bora,upendo na si kuiachia serikali mzigo huo au mashirika yasiyo ya kiserikali tu.
Aidha, Mama Samia ameiomba jamii kuweka mipango mizuri ya kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto yatima kwa kuwa nao wana haki ya kuishi vizuri kama watoto wengine.

b-2
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimpongeza Mboni kwa shughuli hiyo kwani inasadia katika kukumbuka jamii hasa watoto hao ambao wengi wao wanalelewa katika vituo vya Yatima.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE