“Wao wanakaa gesti (nyumba za
kulala wageni) halafu wanawapa viroba watoto wa masikini ili watangulie
kuandamana, sasa mimi nataka watangulie wao halafu waone.”
27 Julai mwaka huu, Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema taifa alitangaza kuwa chama hicho kitafanya
mikutano ya hadhara na maandamano nchi nzima ili kupinga kile
alichokiita udikteta wa serikali ya awamu ya tano.
Hayo yanajiri ikiwa ni saa chache
baada ya Salumu Mwalimu Naibu Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar)
kusisitiza mbele ya waandishiwa habari jijini Dar es salaam kuwa
maazimio ya chama hicho yapo pale pale na kwamba maandalizi ya msingi ya
utekelezaji wake yameanza.
“Hatutarudi nyuma, hatutatishika,
wala hatutatetereka kufanya siasa ni wajibu wetu, siyo hisani ya mtu
mmoja au kikundi cha watu. Ni wajibu wetu, ni haki yetu iliyo ndani ya
sheria inayoongoza vyama vya siasa na kanuni zake,” amesema Mwalimu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment