October 25, 2016

indian-bride-marries-to-the-wedding-guest
Mwanamme mmoja nchini Saudi Arabia ameweka historia kwa kudumu muda mfupi katika ndoa yake baada ya kumpa talaka mkewe saa mbili baada ya ndoa yao.
Wapenzi hao walifunga ndoa hivi karibuni na mwanamme aliamua kutoa talaka kwa mkewe kisa alisambaza picha zao za harusi kwa marafiki zake waliopo Snapchat.
Mwanaume huyo alipopata taarifa kuhusu picha zao kusambazwa Snapchat aliamua kuandika talaka kwa mkewe huyo.
Kwa mujibu wa mwanamme huyo ni kwamba makubaliano yao na mkewe ilikuwa asitumie mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Snapchat au Instagram baada ya harusi yao.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Saudi Arabia ni kwamba hiyo ndiyo ndoa iliyodumu kwa muda mfupi zaidi nchini humo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE