November 08, 2016

14925600_1212604925476524_7426149884218990404_n
Waziri wa zamani na Mbunge wa jimbo la Mufundi Kaskazini Mkoani Iringa, Joseph Mungai amefariki dunia jioni ya leo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya ITV, Mzee Mungai amekutwa na umauti baada ya kuanza kutapika mfululizo, familia imedia kuwa tatizo hilo limemkuta baada ya kudaiwa kula kitu kibaya.

Afisa Uhusiano wa Hospitali wa Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema mwili wa Marehemu Mungai umepokelewa katika idara ya magonjwa ya dharura na kuthibitisha kifo saa 11:20 jioni
Amesema mwili wake umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mwanasiasa huyo mkongwe nchini alikihama chama chake cha CCM na kujiunga na chama cha siasa cha CHADEMA katika harakati za uchaguzi mkuu mwaka 2015.
                        

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE