March 22, 2017

Aliko Dangote 
Aliko Dangote 


Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea mwaka 2017 iliyoandaliwa na jarida la Forbes.
Jarida la Forbes limemtaja mfanyabiashara mashuhuri wa Nigeria Aliko Dangote kuwa bado ndiye mtu tajiri zaidi katika bara la Afrika.
Umeorodhesha utajiri wa Dangote na kukadiria kuwa na thamani ya dola za Kimarekani bilioni 12.2.
Kadhalika Kuna mabilionea 25 mwaka huu barani Afrika ukilinganisha na 24 waliokuwepo 2016. Utajiri wao unapimwa kwa dola za kimarekani.
Image result for dewji
Mohammed Dewji
Ripoti hiyo pia imemtaja Mtanzania Mohammed Dewji kuwa bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa dola bilioni1.09.
Image result for Isabel dos Santos 
Isabel dos Santos
Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria, ndio mabilionea wanawake pekee mwaka huu.
Dangote Dangote, ambaye ni mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kuzalisha saruji Afrika anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.
Dangote pia amewekeza katika kampuni za chumvi, sukari na unga ambazo ni mali yake.
Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na baba yake katika miaka ya 1970.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE