Kama
ni mpenda soka ni lazima utakuwa unavutiwa na shabiki wa zamani wa
Yanga, Ally Yanga kutokana na ushabiki wake kila timu yake ilipocheza.
Yanga
ilimpoteza shabiki wake maarufu, Ally Mohamed ‘Ally Yanga’ ambaye
alifariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Mpwapwa, Dodoma.
Lakini kunaweza kuwa na faraja mpya kwa mashabiki wa Yanga baada ya mrithi wa Ally Yanga kupatikana/
Lakini kunaweza kuwa na faraja mpya kwa mashabiki wa Yanga baada ya mrithi wa Ally Yanga kupatikana/
Shabiki huyo mpya ambaye ameamua kwenda na ule mfumo wa marehemu Ally Yanga katika ushangiliaji, anaitwa Mack.
Mack
ameanza kuonekana kwenye Uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jijini la
Dar es Salaam wakati Yanga ilipoivaa Ruvu Shooting na kupoteza kwa bao
1-0.
“Nilikuwa
shabiki mkubwa sana wa Ally Yanga na baada ya kifo chake niliumia sana,
kwa hiyo ili kumuenzi basi bora niige aina yake ya ushangiliaji wake
kama kumuenzi,” alisema.
Mack
alionekana kuwashitua baadhi ya mashabiki uwanjani pale kwa kuwa
hawakuamini kumuona hadi walipoelezwa kwamba huyo ni shabiki mwingine.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment