August 18, 2017

Image result for Mahakama kuu

(CUF–Chama Cha Wananchi)
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
Mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Ndyansobera leo Ijumaa Tarehe 18/8/2017 kulikuwa na shauri moja lililokuwa linaendelea kusikilizwa ikiwa ni muendelezo wa usikilizaji wa Pingamizi lililowekwa na Walalamkiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Lipumba na Wenzake katika shauri dogo la madai (Miscelleneous Civil Application No. 51/2017) kuhusu maomb ya Zuio kwa Bodi ya Wadhamin ya CUF iliyosajiliwa na RITA kusimama kutekeleza majukumu yake mpaka hapo shauri la Msingi namba 13/2017 litakaposikilizwa na kuamuliwa.
Mheshimwa, Ally Saleh (muombaji/Applicant) amewakilishwa na
1.Mpale Mpoki
3.Loveness
Chama kwa upande wa BODI HALALI YA WADHAMINI YA CUF Itawakilishwa na;
1. Juma Nassor
2. Daimu Halfani
Upande wa Lipumba na Upande wa Wajumbe FEKI wa Bodi iliyosajliwa uliwakilishwa na Majura Magafu na Hosea Chama. Hoja za majibu ya Mapingamizi zimeendelea kutolewa na pande zote mbili na kusikilizwa mpaka saa 10:03 Alasri, Mahakama imepanga kutoa maamuzi Juu ya Pingamizi hizo Tarehe 6 Septemba, 2017.
HOJA KUHUSU SHAURI LA RITA:
Wakili Msomi Mpare Kabe Mpoki alifanya muendelezo wa Msisitizo wa hoja za Wakili Msomi, Fatma Karume na kuongeza nyngine mpya mpya moto moto. Mpoki katika kujibu Hoja alieleza haoni sababu za kujibu Mapingamizi ya WAkili Mashaka Ngole kwa sababu hoja za mapingamizi yake zilikufa zenyewe Jana na kwa kuwa hazikuingizwa katika kumbukumbu ya mahakama. Ameeleza kuwa Kiapo cha Ally Salehe ni Sahihi. Hoja zipo nyingi naomba Tuishie hapa,
KUHUSU SHAURI LA RUZUKU NAMBA 28/2017:
KATIKA hatua nyingine liliitwa shauri tajwa hapo juu mbele ya Jaji Ndyansobera ili litolewe maamuzi kwa kuwa shauri la msingi namba 21/2017 lililoondolewa (Struck Out) Mahakamani hapo Ijumaa wiki iliyopita. Mawakili Wasomi Juma Nassoro, Daimu Halfani, na Hashimu Mziray waliieleza Mahakama kuwa hawakuwa na Taarifa yeyote ya kuitwa kwa Shauri hiyo leo kwa kuwa kwa mara ya mwisho Mahakama ilipanga kulitaja na au kulisikiliza Tarehe 22/8/2017. Wameiomba mahakama ibakie na ratiba hiyo mpaka Jumanne Tarehe 22/8/2017. Jaji Ndtansobera Amekubaliana na hoja za Mawakili Wasomi na kwa msngi huo hakuna Amri yeyote iliyotolewa, zaidi ya kusubiri siku hiyo. Kwa mujibu wa sheria kwa kuwa Shauri la Msingi namba 21/2017 limeondolewa basi na hili huenda Mahakama ikafanya maamuzi hayo siku hiyo ya Jumanne. Mawakili wetu tayari wameshachukua hatua za Kisheria stahiki katka hilo.
Tunarudia tena “The Court Order(s) cannot be given away or Vacated and or nullified by implication. There must be another express order(s) to nullify or to set aside the preceding order(s).
AMRI YA ZUIO LA KUTOTOLEWA KWA FEDHA ZA RUZUKU YA CUF TZS 1.4 BILIONI LIKO PALEPALE MPAKA HAPO MAHAKAMA ITAKAPOTOA AMRI NYINGINE VINGENVYO NA AMRI HIYO KUWASILISHWA KWA MAMLAKA HUSIKA KAMA HAZINA KUU YA SERIKALI, TAASISI ZA FEDHA, MABENKI, MSAJLI WA VYAMA VYA SIASA, NAKADHALIKA NA KUFUATWA KWA TARATIBU ZOTE ZA KIMAHAKAMA. ENDELEENI KUPUUZA TAARIFA ZA KIPROPAGANDA ZINAZOTOLEWA NA WASALITI.
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa leo Tarehe 18/8/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa

SALIM BIMANI
MKURUGENZI-0777414112 / 0655314112

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI
0715 062577 au 0767 062 577
maharagande@gmail.com

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE