August 19, 2017

Image result for Kilwa
Kwa wale wapenzi na mashabiki wa mwana Hip Hop Niki Mbishi, jina la Unju bin Hunuk kwao halitakuwa geni kabisa kwani Niki hupenda sana kumtaja huyu bwana.Unju bin Unuq pia wengine humwita Unju bin Unuku ama Unzi Bin Ununuk) ni jina la jitu katika masimulizi ya wakazi wa pwani ya Tanzania. Hadithi zake zasimuliwa kuanzia Bagamoyo hadi Kilwa.
Historia yake inapatikana katika makumbusho ya Kaole huko Bagamoyo.
Moja ya mambo ya ajabu ya mtu huyu ni urefu wake yaani kimo, inasadikiwa alikuwa na urefu mkubwa ulioweza kumfanya atembee baharini na miguu yake kugusa chini.

Pia alikuwa akitembea kutoka nchi hadi nchi kutokana na urefu wake. Inasimuliwa kuwa moja kati ya nyayo zake inapatikana kwenye jiwe alilokanyaga huko Tabora, wayo wa mguu wa kushoto wakati wayo wa mguu wa kulia ulionekana kwenye jiwe alilokanyaga huko Kongo.
Inasimuliwa pia akitaka kula alikuwa akichukua samaki baharini kwa mkono na kuchoma katika jua kisha anakula.
Kuhusu maisha yake inasimuliwa kuwa Unju bin Unuk hakuoa wala kuolewa kutokana na umbo lake.
Sehemu nyingine ya hadithi yake ni alipokufa Unju bin Unuq, aligawanyika vipandevipande kutokana na urefu wake na inasemekana kidole chake chenye urefu wa kilometa moja kasoro ndicho kilichopatikana na kuzikwa pale Bagamoyo, lakini hakuna simulizi mwili wake uliobaki uliangukia wapi.
Unju bin Unuq alimuwa na ndugu yake aliyejulikana kama Geofrey bin Unuk, huyu alipatikana maeneo ya Dodoma.
Au kwamba Unuq baada ya kupotea kwa muda wa miaka mingi alama zake zimeonekana katika mji wa Dodoma

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE