Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalimu amedai
kuibiwa kwa sanduku la kupigia kura katika Mtaa wa Idrisa Magomeni
Jijini Dar es Salaam.
Salum Mwalimu ameyasema hayo leo wakati akizungumza na mubshara na
kituo cha runinga cha ITV ambapo alisema kuwa alipigiwa simu na Wakala
wake kuwa sanduku limekuja kuibiwa na baadae kurudishwa baada ya dakika
10.
“Nimepigiwa simu na wakala wangu kuwa sanduku lilikuja na kuibwa lakini nikazungumza na msamamizi wa kituo hichi pamoja na Polisi ambae ni msamimizi mkuu wote walikiri kuwa sanduku limeibwa na kwa pamoja wote tulikubaliana kuwa sanduku liliibwa na mtu ambae alikuja na kulipora japo watu walikuwa wamekaa hapa hapa akatokomea nalo”, amesema Salum.
“Baada ya dakika kama 10 hivi sanduku likarudishwa. Sasa kinachonishangaza ni kwamba Polisi na Tume wanasema uchaguzi uendelee.”

0 MAONI YAKO:
Post a Comment