Hatimaye mwili wa mtu mmoja umepatikana ukiwa unaelea kandokando ya mto Kilombero takribani kilometa 5 kutoka eneo kilipozama kivuko cha mto kilombero januari 27 mwaka huu majira ya saa moja na nusu usiku.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema kupatikana kwa mwili huo ni jitihada zinazoendelea kufanyika kivukoni hapo kuhakikisha iwapo kuna miili mingine iliyozama inaopolewa .
Kamanda amemtaja jina la marehemu ayeopolewa kuwa ni Novatus Namali aliyekuwa mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya RAFA ya mjini Ifakara, ikielezwa kuwa serikali inatarajia kutumia helkopta ili kusaidia katika uokoaji .
Mwili wa aliyekuwa mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya RAFA Novatus Namali , umeleta matumaini kwa wananchi wanaosubiri kupatikana kwa miili ya ndugu na jamaa zao waliozama kwenye ajali ya kivuko januari 27 mwaka huu.
Pia Kamanda huyu ametoa onyo kwa vyombo vya habari juu ya upotoshaji wa taarifa za tukio hilo.
Katika hatua nyingine , Melikioli Mwangi , mzazi wa mtoto aliyekuwa mtumishi wa benki ya CRDB Dastun Rwegasira ambaye hajapatika mpaka sasa amesema anasikitishwa sana na tukio hilo kwani limemfanya kuwa katika wakati mgumu
Pia mzazi huyu ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika , juu ya uendeshaji wa vivuko nchini kufanya uchunguzi wa kina kabla chombo hakijaanza safari ili kuweza kuepusha madhara na kusababisha vifo kama hivyo vilivyotokea.
Kivuka cha kilombero 2 kimezama januari 27 mwaka huu majira ya saa moja na nusu usiku kikiwa na abiria ambao idadi yao haikufahamika , magari matatu, pikipiki na ,baskeli pamoja na mizigo mingine yakiwemo magunia ya mpunga.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment