Msanii
Nuh Mziwanda amesema hajutii maisha yake aliyoyapitia akiwa na mpenzi
wake wa zamani, kwani amesha move on (kusonga mbele).
Nuhu
Mziwanda ambaye hivi karibuni ameachia kazi yake ya ‘Jike Shupa’
aliyomshirikisha Ali Kiba, ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye
kipindi cha 5SELEKT cha EATV, na kusema kuwa kwa sasa yeye anachofikiria
ni kazi zaidi.
“Kujuta
kupo lakini sijuti kwa sababu nishaendelea, nimesha move on (songa
mbele ) na maisha yangu na nafanya kazi zangu,” alisema Nuhu Mziwanda.
Pia
Nuhu Mziwanda amezungumzia mahusiano yake ya sasa ambaye amekiri
kufahamiana na mwandani wake huyo kwenye mitandao ya kijamii, na kusema
hataki tena maisha ya mitandaoni kwani alishayapitia, na anachokifanya
kwa sasa ni kubadili status (hadhi) ya maisha yake.
“Sitaki
kuweka mahusiano kwenye media (vyombo vya habari), sawa ni vizuri
ukiamua kuweka wazi, nishapitia sana hayo maisha, nataka kurudisha
status yangu, nimekaa kimya muda nimegundua nina mashabiki wengi, sitaki
maisha ya skendo, sitaki status ya skendo,” alisema Nuhu Mziwanda.





0 MAONI YAKO:
Post a Comment