Msanii
wa filamu nchini Vicent Kigosi amefunguka na kusema kuwa yeye ni msanii
pekee kutoka Tanzania ambaye amechaguliwa kushiriki katika filamu
inayounganisha nchi mbili ya Rwanda na Tanzania.
Ray
Kigosi kupitia mtandao wake wa kijamii aliandika kuwa kwa nafasi
aliyopata hawezi kuwaangusha watanzania kwani yeye amekwenda kuwaonyesha
kazi.
“Nipo
nchini Rwanda nimekuja kushoot movie inayoshirikisha nchi mbili,
Tanzania na Rwanda ni msanii pekee toka Tanzania niliyechaguliwa kuja
kufanya movie hapa nchini Rwanda nina imani sitowaangusha watanzania
wenzangu hapa ni kazi tu” aliandika Ray Kigosi





0 MAONI YAKO:
Post a Comment