MAGARI YENYE PICHA YA RAIS YAKAMATWA
Licha ya rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta kuruhusu magari yanayobeba abiria nchini Kenya kuchorwa ama
hata kupaka rangi yoyote ile,mabasi mawili yaliochorwa picha yake
yamekamatwa na maafisa wa polisi mjini Mombasa Kenya.
Maafisa wa
trafiki mjini Mombasa waliyakagua magari hayo na kuyakamata magari yote
yaliokuwa yamechorwa picha pamoja na magari yenye madirisha yasioonyesha
ndani.
Magari sita yakiwemo mawili yaliokuwa na picha ya Uhuru
yalikamatwa,licha ya agizo la rais kuruhusu wamiliki wa matatu kuchora
picha katika magari.
Uhuru alikuwa amesema kuwa hatua hiyo itawasaidia vijana kutumia vipaji vyao ili kuweza kujinufaisha kimaisha.
Uchoraji katika magari hayo na muziki ulipigwa marufuku mnamo mwaka 2003 na aliyekuwa waziri wa uchukuzi John Michuki.
No comments:
Post a Comment