September 18, 2012

Na
       Ngwesa
AFANDE SELE

SI VEMA kutumia lugha za dhihaka na kejeli kwa mtu kupitia mtandao/magazeti wakati wewe mwenyewe hutumii jina lako halisi ili nawe kila mtu akutambue/akuchambue! Vema si kutumia Udhaifu wa umaarufu wa Sele kunitusi kwa mambo ya kipuuzi tu; ambayo hata kama nimekosea ungepaswa kunielimisha na sio kunibeza na kutukana, ukizingatia kuwa HAKUNA BINADAMU ALIKAMILIKA.

AFANDE SELE AKIWA NA MWANAE TUNDAJEMA
NB; Bukta,vibwaya n.k ni sehemu ya burudani na bangi hata wabunge mawaziri na nchi kibao wanatumia, SEMA TATIZO LA WATANZANIA WENGI HASA VIONGOZI NI UNAFIKI WETU TU WA KUTOKIRI UDHAIFU WETU, NA NDIO MAANA HATA RUSHWA HAITOKWISH KWA KUWA KILA MTU ANAILAANI RUSHWA, LAKINI NYUMA YA PAZIA WENGI WETU VIONGOZI MPAKA RAIA WANAPOKEA, NA KUTOA RUSHWA, katika maisha ya kila mtu Bangi=pombe =sigara= uzinzi=ufisadi VYOTE NI VIBAYA, lakini ajabu mzinzi, mlevi, fisadi wote hao wanambeza mvuta bangi wakati na wao SI WASAFI KIMAADILI, na pia tujenge utamaduni wa KUPINGANA BILA KUTUKANA na sisi wote ni wanandugu, na kila mmoja ana mapungufu yake? YUPI ASIE NA DOA?

 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE