November 27, 2012

                                                            Marehemu   enzi  za  uhai  wake
Jan  usiku  zilitapakaa  habari  kuhusu  kifo  cha  msanii  wa   BONGO Freva   na  tasnia  ya  Filamu  maarufu  kwa  jina  la  Sharo  Milionea
  Kufikia  majira  ya  saa  tano  kasoro usiku  Kamanda  wa  Polisi  mkoa  wa  Tanga alitibisha   taarifa  hizo  kupita    kipindi  cha  ALA ZA  ROHO kinachorushwa  na kituo  cha  Clouds  fm chini  ya  mwana  dada  DIVA. Kamanda kizungumza  na  Suody Brown  alisema
  '' “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe''

                                                                     Pumzika  kwa  amani Sharo   Milionea 

Tumeshindwa  kuweka  picha  za  mwili  wa  Marehemu   kutokana  na  sababu  muhimu   za  kibin  adam.  Samahini  kwa  ilo.

                                   Gari  ya  Sharo  Milionea  baada  ya  ajali


0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE