February 27, 2013

 
Joel   Kusaga  ( Mr  jo)



Luge  Mutahaba

   Siku Moja baada ya Kituo cha Redio cha CLOUDS FM kushinda tuzo ya Ubora wa bidhaa, maarufu kama SUPER BRAND upande wa vituo vya Redio nchini, Uongozi wa CLOUDS MEDIA GROUP umeandaa kampeni maalum ya kuhamasisha uzalendo kwa Watanzania, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha jamii umuhimu wa kuthamini na kuipenda nchini yao katika masuala mbalimbali.
Akizungumza kwenye kipindi cha POWER BREAKFAST kinachorushwa na kituo cha CLOUDS FM, Mkurugenzi Mtendaji wa CLOUDS MEDIA GROUP, JOSEPH KUSAGA, amesema lengo la kampeni hiyo ni itakayoanza March 8 mwaka huu, ni kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa kutumia bidhaa za hapa nchini sambamba na kuonyesha uzalendo katika masuala mbalimbali.
  
  Aidha KUSAGA amebainisha kuwa katika Kampeni hizo viongozi na Wafanyakazi wote wa CLOUDS MEDIA GROUP, watashiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kushiriki kikamilifu kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, kwa kutoa tuzo kwa Wanawake mbalimbali walioifanyia mema Tanzania katika shughuli zao mbalimbali.
Katika hatua nyingine KUSSAGA ameuelezea mfumo mpya wa kisasa wa urushaji matangazo ya Televisheni nchini na kubainisha kuwa tangu mfumo huo ulipoanza rasmi Januari Mosi Mwaka huu, umechangia kwa kiasi kikubwa kushusha thamani ya Soko la biashara ya Matangazo ya runinga, kutokana na vituo vingi kupoteza idadi ya Wadhamini

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE