Kufuatia ajali iliyotoke jana Asubuhi kwa kudondoka kwa ukuta wa Ghorofa lenye zaidi ya ghorofa 14 na kusababisha vifo vya watu wengi jijini Dar es Salaam katika makutano ya Barabara ya Gandira Gandi na Morogoro, msanii wa muziki wa kizazi kipya toka Moro mwana dada Dayna Nyange, amefunguka kwa kuzungumzia vifo hivyo>
Akizungumza kwa njia ya simu na ubalozini.blogspot.com, Dayna amesema ni kitendo cha kusikitisha kwa kupoteza ndugu zetu bila kutarajia
'' kwa kweli inasikitisha san kwa kupata taarifa kama hiyo ya vicho vya watu wengi tena kwa pamoja, kinachotakiwa sasa ni kuwaombnea hao waliotangulia ili wapate mapumziko yaliyo mema lakini inaum sana''
Pia Dayna anayetamba na wimbo wake mpya kwa sasa wa LEO alioimba na Mr: Blue, amefunguka kwa kusema ajalim haina kinga, ila ajali kama hiyo inahitaji uchunguzi wa kina na kama watapatikana wahusika na kubainika kuna uzembe wa kitaalamu, basi wanastahili kuchukuliwa ahtua kali za kisheria.
Blog hii pia inawatakia mapumziko mema ndugu zetu waliotangulia mbele za haki.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment