March 08, 2013

Dayna   Nyange
 
 
 
     Leo  ni  tarehe  8/3.  siku    ya  leo  kila  mwaka   wanawake  Duniani  wanaadhimisha  siku  ya  wanawake  Duniani..  Sherehe   mbalimbali zinafanyika,  maandamano, makongamano   na  watu  hutumiana  ujumbe  kuhamasisha  juu  ya  haki  za  wanawake.  Watu  mbalimbali hutoa  zawadi  kwa  wanawwake  na  ujumbe  kuwatumia.  Mwanamuziki  toka  mkoani  Morogoro  Dayna  Nyange,  kupitia  siku  ya  wanawake  duniani  ameamua  kutoa  yake  kwa  wanawake  wenzia  na  jamii  kwa  jumla
 
     " Naitwa dayna nyange. mwanamuziki wa bongo freva. ni mwanamke wa kitanzania. naungana na wanawake wengne duniani kote ktk kuhadhmisha cku ya wanawake duniani.  Nawashauri wanawake wenzangu juu ya kuji2ma kufanya kaz ili kujipatia maendeleo bila kutegemea wanaume. Naamini  wenyewe 2naweza  tena bila ata ya kuwezeshwa.  Nakupitia siku hii muhmu kwetu. naiomba serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhakikisha inapambana vilivyo juu ya unyanyasaji wa kijinsia  tunaoupata wanawake. hasa ubakaji, ukeketaji na  mauaji yanayoendelea zidi  yetu, tunaiomba serikali ihakikishe kwamba wahusika wa matukio kama hayo wanachukuliwa hatua za haraka ili kukomesha maovu hayo. pia nijukumu la kila mwanamke na   Niwajibu wetu kina mama pia na jamii kwa jumla kupambana na majanga haya. tushikamane kujiletea. Tupendandane tushikamane WANAWAKE TUNAWEZA.  by dayna nyange".

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE