ZITTO KABWE-MB
Mbunge kutoka Kigoma Kaskazini - CHADEMA Zitto Zuberi Kabwe, kesho anataraji kupeleka kilio cha unyonyaji wa kazi za wasanii na jinsi ingewezekana kuwasaidia.
Mbunge huyo machachari na chaguo la vijana wengi hasa wapenda mabadiliko, amefunguka kupitia katika ukurasa wake wa facebook uku ikionekana wadau mbalimbali kuchangia
#RBT
biashara ya kuuza kazi za sanaa mfano nyimbo kama miito ya simu ie
#Ringtones imeshamiri sana nchini. Unataka kujua biashara hii inaingizia
mapato kiasi gani kampuni za simu (Network Providers), wachuuzi ama
content providers/content aggregators na wasanii (content creators)?
Unataka kujua Ni namna gani biashara hii ingeweza kuwa mkombozi wa
wasanii wetu Kwa kuwaongezea kipato na hivyo kuongeza ajira nchini
lakini imekuwa mnyonyaji mkubwa wa jasho la wasanii kwa kuwagawia mapato
kiduchu? Unataka kujua hatua tunazopendekeza ili kuhakikisha kuna
#Uwazi katika biashara hii na mgawo wa mapato unakuwa wa haki Kwa wadau
wote yaani wasanii na kampuni za simu? Basi fuatilia kikao cha #Bunge
cha kesho tarehe 9 Aprili 2013 kuanzia saa Tatu kamili asubuhi ambapo
Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia itajibu
swali la msingi na maswali ya nyongeza kuhusu biashara ya #RBT . Pia
utajua kuhusu wimbo 1 tu wa #Kesho ulinunuliwa na watu wangapi katika
mwezi mmoja tu wa January 2013 na mtunzi wa wimbo huo alipata mapato
kiasi gani dhidi ya mapato waliopata makampuni ya simu na content
providers wenye mkataba na msanii huyo. Wajibu wa kulinda wanyonge dhidi
ya wenye Nguvu Ni wajibu wa Dola. Sasa Ni mwendo wa #Uwazi na
#MapatoYaHaki katika kazi za Sanaa nchini kwetu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment