May 21, 2013

Dayna  Nyange
   Leo ni miaka 17 tangu kutokea kuzama kwa  meli  ya MV Bukoba katika ziwa Victoria na kusababisha maafa makubwa kwa  ndugu zetun waliokuwamo katika meli ile. 
   Katika kumbukumbu hizo, baadhi ya wasanii wa bongo freva wamezungumzia na kuonesha kusikitishwa kwao kwa tukio lile, lililopoteza watanzania wengi mnamo tarehe 21 mei 1996.

  Msanii wa kike toka  Morogoro  Dayna  Nyange mkali wao, ameandika katika  ukurasa wa Facebok kwa majonzi na kutoa mtazamo wake kwaserikali

KIfo ni hatua ya mwisho ya maisha ya mwanadam. leo n miaka 17 imetimu tangu taifa lipate pigo pgo la kuondokewa na ndugu zetu ktk ajali ya meli ya Mv bukoba ktk ziwa victoria. cku kama ya leo 2kiwa kama watanzania kila mmoja kwa imani yake ni jukumu la kufanya moambi juu ya marehemu wote waliohusika ktk ajali ile ya kutisha. tuliwapenda ila mungu kawapenda zaidi. ushauri wangu kwa serikali, itengwe cku maalum ya kuwafanyia maombi ya pamoja ndugu zetu wale. ulikuwa mcba wa kutisha sana kwa taiifa letu ambayo bnafsi ajali ile siwez kuisahau. ee mungu wapumzshe ndugu zetu mahala pema peponi. __ SL8.IT for Blackberry. Ameandika Dayna na  watu  kadhaa wakichangia.
 
Shilole
SHILOLE:   Inasikitisha sana kwa kweli lakini haina jinsi, kilichotokea  kilituumiza  wengi sana, lakini kazi ya mungu haina makosa.  Tunashkuru kila analotenda japo mengine  yanaumiza kama hili la kuondokewa na ndugu na jamaa,  wapo walioondokewa na wazazi wao, ila mungu amepanga, niwaombe watanzania wenzangu, kikubwa ni kuwakumbuka kwa duwa na ubani ili mungu awapunguzie adhabu. Inasikitisha sana ukifikilia ajali jinsi ilivyotokea na taarifa tulizokuja kupata. Mungu awarehemu  marehemu wote.
   
Koba Mc
KOBA MC : Tusikumbuke machungu yaliyopita maana tutazidi kuumia na hatutafanya kitu. Lakini hili la ajali ya ndugu zetu waliopotea tena majini< hujui kamawengine wameliwa na samaki au na viumbe vya majini, inauma sana. nakumbuka nilikuwa nasoma wakati ule bado umri mdogo, sikujua maumivu yake lakini ninavyozidi kukua na na fikra zinatanuka, kwa kweli ilikuwa baraha,  cha msingi tuzidi kufanya maombi juu ya ndugu zetu wale, mbele wao sisi nyuma na hatujui tutakufa kwa kifo kipi. Tumwachie mungu mwenyewe.
 
Blog hii  na watanzania wengine, tunaomba kufanya ibada kwaajili ya ndugu zetu. amin

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE