Baada ya kushinda tuzo ya Best African act kwenye BET awards,
kumefungua njia nyingi za Ice Prince ambaye anawakilisha Nigeria. Meek
Mell msanii ambaye ni mshirika wa karibu na mkali wa FIesta 2012 Rick
Ross, amempa mualiko Ice Prince wa kwenda kwenye jiji la Philadelphia
ku-perform kwenye jukwaa moja ambalo litashambuliwa na mastaa kibao
wakiwemo kutoka MMG.
Tarehe 30/8 kutakuwa na tamasha ambalo
litawakutanisha watu mashuhuri tofauti kutoka kwenye michezo na muziki
ambapo ndipo Ice Prince ataperform mbele yao.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment