
Huku Tanzania ikiendelea kusuasua kila mwaka wa mashindano ya Miss
World, mrembo wa Philippines Megan Young.
Megan ,23, ametwaa taji hilo licha ya maandamano makubwa
yaliyofanywa na waislamu wakipinga kufanyika kwa mashindano hayo ambayo
yalifanyika chini ya ulinzi mkali.


Mashindano hayo yalifanyika katika kisiwa cha Bali nchini
Indonesia na waislamu walipinga kwa maandamano kwamba yanakiuka maadili ya dini
yao.



Megan aliwashinda wasichana wengine 127 ili kutwaa taji hilo huku nafasi ya pili ikienda kwa Miss France Marine Lorphelin na mrembo kutoka Ghana Carranzar Naa Okailey akatwaa nafasi ya tatu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment