October 09, 2013

Rapper Nay Wa Mitego amesema amekuwa akisumbuliwa mno na maafisa usalama pamoja na vyombo mbalimbali vya habari wanaomdhania kuwa anajihusisha na biashara ya madaya ya kulevya kitu ambacho amekuwa akikanusha kwamba sio kweli.

Akiongea na Bongo5 leo kwa njia simu Nay amesema anasikitishwa kupokea taarifa zinazodai kuwa anajihusisha na biashara hiyo haramu, kitu ambacho hakifanyi kwakuwa anategemea shughuli zake za muziki zinazomlipa vizuri.

“Watu wamekuwa wakishangaa sifanyi show hata mwaka mzima lakini maisha yanaenda namiliki gari ndio maana wanaongea mengi huku media na maafisa usalama wananichunguza kila siku,” alisema Nay.

Pia msanii huyo wa Salam Zao, amesema yupo kwenye maongezi na kampuni ya simu ili imfanye kama balozi wake.


“Nasubiria mambo yangu yaende poa, nimeingia mkataba wa kuwa balozi wa mtandao wa simu hapa nchini bado muda wake kuuweka wazi kwasababu tupo kwenye makubaliano zaidi na pia ikifika muda nataka kuanika vyanzo vyangu vyote vya mapato, ” alisema

Related Posts:

  • Unique Sisters warudi kwako wewe    Wasanii wakongwe kwenye game ya muziki ambao ni ndugu wa familia moja Unique Sisters, wamesema wamerudi rasmi kwenye game, kutokana na maombi ya mashabiki na kuachia kazi yao mpya kwa ajili yao inayoitwa '… Read More
  • Ancelotti atimuliwa Bayern   Kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti amefutwa kazi leo kufuatia mwanzo mgumu wa msimu wa 2017/18 yakiwemo matokeo ya jana usiku ambapo timu hiyo ilikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa PSG. Mkurugenzi … Read More
  • Mbowe Anyang'anywa Gari Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kimesikitishwa na hatua ya uongozi wa Bunge la Tanzania ya kulichukua gari la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe alilokuwa akilitumia kwa sh… Read More
  • Watanzania hawatatuelewa - Mwakyembe   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa endapo watashindwa kufanya maandalizi mazuri ya michuano ya mataifa ya Africa (AFCON) kwa vijana 2019 basi Watanzani… Read More
  • Mama yake Hayati Samuel Sitta Alipoikaribisha Tigo Fiesta Tabora   Kama ilivyo kawaida ya FIESTA, huambatana na matukio mbalimbali ya Kitaifa, Kwa mkoa wa Tabpora watasherehekea Fiesta siku ya Ijumaa 01 Oct .Geah Habib alipata nafasi ya kutembelea nyumbani kwa Hayati Spika wa B… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE