January 08, 2014

Hit maker wa 'Mrs Super Stars' Young Killer Msodoki yupo njiani kuachia wimbo mpya 'My Power' aliyomshirikisha msanii wa RNB Damian Soul mwishoni mwa mwezi huu wa Januari.
Akizungumza na tovuti ya 100.5 Times Fm amesema wimbo umetengenezwa kwenye studio ya Classic Sounds iliyo chini ya producer Mona Gangsta.
'Muziki ni mapambano, Kwenye imla mi silembi..mwandiko,Msuri tembo..matokeo..sungura....ndo maana ya msuri tembo matokeo sungura,ni wimbo wangu mpya 'My Power' niliyomshirikisha Damian Soul,shughuli zote za kuandaa wimbo huo zimefanyika Classic Sound chini ya producer Mona Gangsta,natarajia kuachia hewani mwishoni mwa mwezi huu,mashabiki wa msodoki mkae mkao wa kula,mimi silembi'Alisema Young Killer.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE