Kampuni
ya Visual Unity Global yaingia mkataba na Clouds Media Group
ilikuwezesha jamii kuona matangazo Ya redio kwa njia ya video kupitia
kwenye mitandao.Visual Unity Global yaendelea kupanua huduma zake za
vuMobile baada ya kusaini mkataba mpya barani Afrika na kampuni ya
nchini Tanzania ya Clouds Media Group.Lengo la uhusiano huu likiwa
ni kuwezesha jamii kuweza kuona matangazo ya redio kwa njia ya video
kupitia kwenye mitandao mahali popote, muda wowote na kukitumia kifaa
chochote.Mkurugenzi Mtendaji wa Visual Unity Global,Tomas
Petru,alisema: “Kwa kushirikiana na Clouds Media tutasaidia kukua kwa
haraka njia ya kupata matangazo ya redio kwa njia ya mtandao nchini
Tanzania.”Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph
Kusaga,alisema kuwa “Ushirikiano huo na Visual Unity Global utasaidia
kuleta na kukua kwa teknolojia ya kisasa nchini Tanzania ili kuweza
kuwanufaisha wateja na wasikilizaji wetu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment