February 06, 2014

Bunge la Tanzania
Serikali ya Tanzania imekanusha taarifa za vyombo vya habari zilizodai kuwa wabunge wa nchi hiyo watalipwa kiasi cha zaidi ya dola laki moja za kimarekani watakapomaliza muda wao wa kipindi cha miaka mitano yakiwa malipo ya kiinua mgongo.
Taarifa ya wizara ya fedha imesema habari hiyo ni ya upotoshaji kwa kuwa Waziri wa fedha ,hakuwahi kuzungumza na mwandishi yeyote kama inavyodaiwa kuwa alithibitisha taarifa hizo.
Baada ya kuzuka kwa taarifa hizo baadhi ya wabunge waliozungumza na vyombo vya habari walikiri kuwepo kwa mipango hiyo huku wengine wakikanusha kuwa hawajawahi kupitisha mapendekezo kama hayo bungeni.
Naye naibu spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameiambia BBC kuwa habari hizi si za kweli '' nipende kusema kuwa jambo hilo kwa kweli si la kweli.Si la kweli kwa sehemu mbili,kwanza kwa utaratibu wa utawala wetu bora Tanzania, hakuna mtu mwenye mamlaka ya kujiongezea yeye mwenyewe kipato chake katika utumishi wa uma.kila ambaye ana mshahara au marupurupu ya aina fulani lazima yaidhinishwe na mamlaka au chombo kingine, ndio utaratibu wa utawala wetu.Kwa hiyo na sisi Bunge hatuna mamlaka ya kujipangia posho ya aina yoyoyte au mshahara wa aina yoyote kwa wabunge au viongozi wa Bunge''.
Pia naibu spika Ndugai amesema madai ya baadhi ya Wabunge kuwa kulikuwa na mpango huo si ya kweli na hayajawahi kujadiliwa katika Bunge hilo.
Taarifa hizo zilisababisha malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu hatua ya serikali kuwapatia wabunge kiasi hicho kikubwa cha fedha huku ikidai kuwa haina fedha za kutekeleza miradi kwa ajili ya huduma nyingine za umma.
CHANZO bbcswahili.com

Related Posts:

  • Mbunge CHADEMA na wenzake, wajiunga CCM   Aliyekua mgombea Ubunge  wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Jimbo la Mvomero mwaka 2015, Mchungaji wa kanisa la Assemblies of God, Oswald Mlay na wenzake wawili wameamua kurejea chama cha mapinduzi … Read More
  • UREMBO:Magese aahidi ushirikiano na Serikali kusaidia vipaji Mkurugenzi wa Kampuni ya Millen Magese Group (MMG), Millen Magese  ameishukuru Serikali kupitia kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye, huku akifurahishwa na uwakilishi mzuri … Read More
  • Diwani wa CHADEMA ahamia CCM Kushoto ni Diwani wa kata ya Shule ya Tanga iliyopo Songea mjini mkoani Ruvuma kupitia tiketi ya Chama Cha Demoklasia na Maendeleo ( CHADEMA )Mussa Ndomba aliyejivua uaanachama na kujiunga Chama tawala cha mapi… Read More
  • Simba yamnasa kipa wa Medeama Kipa wa Medeama, Daniel Agyei ametua nchini tayari kumalizana na Simba. Kipa wa Medeama, Daniel Agyei ametua nchini tayari kumalizana na Simba. Lakini kwa hali inavyoonekana, huenda Simba imeishamaliza kila kitu kwa… Read More
  • Usajili Dirisha Dogo: Mrisho Ngasa atua Mbeya City Picha inayo-trend kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni ya Mrisho Ngasa na afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten ambayo inaashiria tayari nyota huyo wa zamani wa Yanga ameshakamilisha deal na ‘wagonga nyundo wa Mbeya’ … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE