February 01, 2014

  Kufuatia taarifa za Ziotto Kabwe kufanya mikutano nchi nzima  kuijibu CHADEMA ,  Mbunge huyo machachari Bungeni amekanusha taarifa izo.
  Mwanasheria wa Zitto Msomi Alberto Msando ameandika katika ukurasa wake wa facebook 

Conversations with The People tour need no chopper but physical connection with people, discuss with them, eat with them, get angry with them, laugh with them and sleep where they sleep. That's a listening tour. That's transformative politics far away from hate spreading and peddling lies. Inspiration from manipulation.
Upotoshaji dhidi ya Mh. Zitto Kabwe (MB).

Kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwamba Mh. Zitto Kabwe anatarajia kuzunguka nchi nzima kwa kile kinachodaiwa ni 'kujibu mapigo' ya ziara ya Chama mikoani ambayo inaendelea.

Pia taarifa hizo zinadai kwamba Mh. Zitto Kabwe atatumia helkopta kuzunguka kwa msaada wa CCM. Vile vile kuna taarifa kwamba kwenye ziara hiyo Mh. Zitto Kabwe ataongozana na Wabunge sita wa Chadema na watatu wa CCM.

Napenda kuchukua nafasi hii kuelezea umma kuwa taarifa hizo ni uongo na uzushi ambao wanaosambaza wanaendeleza nia ovu kumchafua kwa sababu wanazozijua wao. Ni upuuzi kusema kwamba CCM watamsaidia Mh. Zitto Kabwe kufanya ziara au wabunge wake watamsindikiza. Ni wazi kabisa baadhi ya watu wamedhamiria kumjengea chuki kwa kutaka umma uamini kwamba CCM inamtumia jambo ambalo halina ukweli wowote.

Mh. Zitto Kabwe hajapanga kufanya ziara yeyote mikoani. Mh. Zitto Kabwe hana sababu yoyote ya kufanya hivyo. Taarifa hizo zipuuzwe.

Binafsi anaamini kwamba kuna mambo mengi na ya muhimu ambayo kama kiongozi anatakiwa kuyafanyia kazi badala ya kufanya ziara kama hizi ambazo hazina tija wala manufaa kwa Chama au taifa letu zaidi ya kuharibu chama na kuchafuana.

Shutuma zozote ambazo zinaelekezwa kwake atazijibu kwa wakati ili wananchi watambue ukweli wa yote yanayoendelea baada ya shauri lake kumalizika mahakamani. Endapo Mh. Zitto Kabwe atahitajika kufanya ziara basi taarifa rasmi itatolewa

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE