March 29, 2014

Afande Sele The'King
  Kuhusiana na mambo yanavyokwenda ndivyo sivyo juu ya mchakato wa kupata katiba mpya, uku kila kundi likilia kwa upande wake, Msanii wa muziki wa Hip Hop toka mkoani Morogoro, Afande Sele Mfalme, ametoa lake la moyoni kupitia A/C yake ya  Facebook.
Wkt ukifika nasi tutatoa maoni yetu ingawa wasanii tumetengwa kwa maana ya kukosa muwakilishi ktk bunge maalum la katiba lkn kwangu mimi kama afande sele hii imenipa maana kuwa jk na ccm yake wanachezea akili,miili na rasilimali za watz kitotototo tu huku wakijua hawana nia njema na ya dhati ya kuwapa watz katiba waitakayo bali katiba ya ccm,ndio maana mimi naliita bunge hili ni bunge maalum la kuiba si la katba na kwa jins watz wa sasa walivyoamka na wanavyofuatilia ule ujinga unaoendelea pale dom huenda mchakato huu ndio ukawa mwanzo wa machafuko ktk taifa na mwisho wa jamhuri ya muungano wa tz kwa maana ya kufufuka kwa taifa huru la tanganyika kama ilivyo kwa taifa huru la zanzibar kwa vile ktk mazingira yeyote yale hakuna raia atakaekubali mapendekezo ya ccm badala ya maoni ya wengi yaliyomo kwenye rasimu ya jaji warioba,umimi,uchoyo,woga,ujinga,uroho wa madaraka wa ccm ndio utakaoligawa taifa hili,mtu kijiweni anakwenda bungeni anatoa hotuba kama'juha'tu ''ooh mimi nataka serekali mbili,serekali tatu ktk utawala wangu haiwezekani labda mpaka niondoke madarakani''sasa kama ulikuwa unajua na unataka iwe hivyo kwanini uliunda tume ya warioba na zaid kwanini ulikubali mapendekezo ya tume hiyo ambayo ulikuwa ukikutana nayo mara kwa mara na kupata maelezo yake ambayo ni maoni ya watz walio wengi ikiwemo mfumo wa kutaka serekali tatu ambazo baadae unakwenda kuzikataa mbele ya bunge uliloliunda na kuteua wajumbe wewe mwenyewe?kama ulikuwa na maoni kwanini hukuyatoa mapema mbele ya tume uliyoiteua mwenyewe na iliyogharimu muda na mabilion ya pesa za walipa kod badala ya kwenda kuyatoa bungeni huoni kama ni uvunjaj mkuu wa katiba na uhujumu mkubwa wa uchumi kwa kuwa hilo bunge lako la wez uliloteua linafilisi nchi yenye matatizo lukuki ya kijamii huku likiigiza badala ya kutimiza matakwa ya wengi?kila kitu kimekushinda ktk utawala wako nchi imeyumba iko hoi ufisad ukitamalaki kila mahali ukiongozwa na maswhiba wako sifa pekee tulitegemea sisi ndgzo ingekupa heshima kidogo ni kuliachia taifa katiba mpya safi iliyotokana na matakwa ya walio wengi lkn nalo tayari limekushinda kwa kuendekeza uchama badala ya utaifa sasa utakumbukwa kwa lipi wewe ndg?bora Uzee kuliko Uzembe,hizi ni salam zangu kwako''mjomba'',Ushaharibu,,,,,,,

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE