April 15, 2014

 

Ukraine leo imefutilia mbali uwezakano wa kufanyika mazungumzo yoyote yanayohusu "masuala yake ya ndani" katika mkutano unaopangwa Alhamisi wiki hii unaozileta pamoja Urusi, Marekani na Umoja wa Ulaya, wakati kukiwa na mvutano unaoongezeka baina ya Ukraine na wanamgambo wanaoiunga mkono Urusi. Yurii Klimenko, balozi wa Ukraine katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva ambako ndiko kutakakofanyika mkutano huo, amesema lengo kuu la mazungumzo hayo ni kupanga namna ya kupunguza hofu na kutafuta njia madhubuti za kuitulizua hali hiyo.
Urusi imesema wanaharakati wanaoiunga mkono nchi hiyo ni lazima washirikishwe katika mkutano huo, ambao unaashiria juhudi mpya za kidiplomasia zenye lengo la kuondoa wasiwasi baina ya serikali ya Ukraine inayoungwa mkono na nchi za magharibi na Urusi ambao umesababisha mgogoro mkubwa zaidi wa kiusalama kuwahi kutokea barani Ulaya kwa miongo kadhaa.

Source: dw.de

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE