
Msanii mkongwe Mr Nice amepata ajali jana akiwa ndani ya bajaji
akiwa na abiria mwenzake ndani ya bajaji hiyo. Jinsi ajali hiyo
ilivyotokea kuna gari ‘liliwachomekea’ na dereva wa Bajaji hiyo akaamua
kuikwepesha na kugonga mti. Hali ya Mr Nice sio nzuri sana,kwani
amevimba kichwa na kuumia sana sehemu za usoni na abiria mwenzake ambaye
hajafahamika jina alifariki papo hapo na dereva wa bajaji hali yake sio
nzuri. Chanzo cha ajali hiyo huenda ikawa ni mvua zinazoendelea
kunyesha jijini Dar es Salaam
0 MAONI YAKO:
Post a Comment