Kituo
cha Watoto Yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo leo April
05 wamepata michango mbalimbali toka kwa project yake ya Diva Giving For
Charity ambayo inasimamiwa na Diva wa Ala za Roho ya Clouds Fm.
Huu
ni mwaka wa tatu mfululizo kwa Diva kutoa misaada kwa vituo mbalimbali
vya watoto yatima na mpaka sasa vituo walivyotoa msaada ni pamoja na
Al-madina Children Home Tandale,New Life Home Orphans Home Kigogo na
Makorora Hospitali ya Tanga.
Michango
iliyotolewa leo ni pamoja na Vyakula,vifaa vya elimu kama madaftari
pen,penseli na Milion 1 kutoka Diva’s Wild Events Company,Albert Msando
ametoa Dolar 500 Cash na vifaa vya watu mbalimbali vilivyochangwa na
wadau mbalimbali wa Clouds Fm ambao baadhi yao walijumuika kuonyesha
uzalendo na kusambaza upendo.
Hizi ni baadhi ya picha za kwenye utoaji wa michango hiyo.
Hapa Diva akiwa kambeba mtoto Sauda mwenye matundu matatu katika moyo, anahitaji msaada wa kwenda nchini India kwa matibabu
0 MAONI YAKO:
Post a Comment