Bunge
la bajeti linaendelea Dodoma Tanzania ambapo leo May
27 2014 kwenye kipindi cha maswali na majibu asubuhi, moja ya majibu
yaliyotolewa ni kuhusu uwepo wa mbio za mwenge na gharama zake.
Naibu waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia amesema ‘serikali kuu hutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji na gharama halisi ya wakati husika ambapo mwaka 2012 jumla ya shilingi milioni mia sita hamsini (650) zilitengwa kwa ajili ya kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na kati ya hizo milioni 450 zilitumiwa na Wizara na milioni 200 zilitumiwa na mkoa uliokua mwenyeji wa sherehe za kilele’
‘Kuhusu kiasi cha fedha kinachotumiwa na wilaya, ni kwamba zinatofautiana kulingana na michango ya Wananchi katika wilaya husika kwani michango hiyo ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo huzinduliwa wakati ya mbio za mwenge, kwa ujumla mwaka 2012 Wananchi walichangia zaidi ya BILIONI 11 na milioni 500′

‘Halmashauri
za wilaya na manispaa zilichangia shilingi BILIONI 45, Wahisani na watu
binafsi walichangia zaidi ya shilingi milioni 52 ambapo faida
zinazopatikana kutokana na Mwenge wa Uhuru nchini ni pamoja na kuendelea
kutunza historia na falsafa ya ukombozi wa taifa letu, kuhamasisha
Wananchi kuhusu umuhimu wa kuendelea kuenzi amani, mshikamano, upendo na
zaidi kupambana na ubaguzi wa dini, rangi au ukabila’
‘Mbio za mwenge wa uhuru hutumika kuhimiza miradi mbalimbali kwa njia
ya kuweka mawe ya msingi au kuzindua miradi iliyowekewa jiwe la msingi
mwaka uliopita na pia kuhamasisha moyo wa Wazalendo na kujitolea kwa
vijana hasa kuonyesha umuhimu na nafasi yao katika kudumisha nchi yao,
kulinda uhuru na kuleta maendeleo ya nchi yao’
Baada ya kusoma haya yaliyosemwa na Naibu waziri wa habari Juma
Nkamia leo May 27 2014 bungeni, unalolote la kuchangia? mtazamo wako kwa
ujumla niachie hapa chini kwenye comment mtu wangu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment