
Uvitaji wa Shisha ni sawa na uvutaji wa sigara kulingana na madaktari
Waziri wa afya nchini Tanzania,
amesema kuwa Tanzania inapanga kutathmini sheria ya sasa kuhusu
matumizi ya Sisha ili kufanya mageuzi au kubadili sheria hiyo matumizi
ya Shisha.
Dkt Seif Rashid Selemani amesema kuwa sheria
hiyo italenga kulinda afya ya watanzania hasa walio na uraibu wa Shisha
na pia kuhakikisha kuwa wanaotumia Shisha katika sehemu zengine duniani
wanapata kubadili mfumo wa maisha ili kulinda afya zao.
Hii ni baada ya taarifa ya awali
kuwa serikali ilikuwa tayari imechukua hatua kupiga marufu bidhaa hiyo
ambayo inaenziwa sana hasa na vijana.
Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye
ladha tofauti tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa
mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana mjini Dar
Es Salaam.
Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.
Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.
Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha
wakisema kuwa waraibu wanakabiliwa na tisho la kuugua Saratani sawa na
hatari inayowakabili wavutaji wa sigara.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment