July 20, 2014

 
 MWANAMUZIKI maarufu nchini Uganda, Juliana Kanyomozi, leo asubuhi amempoteza mwanaye wa kiume, Keron (11) aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu. Keron amefariki akiwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, Kenya alipokuwa akitibiwa.
 
 
Juliana akiwa na mwanaye Keron enzi za uhai wake.

Taarifa iliyotolewa katika ukurasa wa Facebook wa Fenon Records inayofanya kazi na staa huyo ilisema:
"Mtoto pekee wa Juliana, Keron amefariki dunia akiwa Aga Khan, Nairobi alipokuwa akitibiwa. Salamu zetu za rambirambi zimwendee Juliana na familia yake katika kipindi hiki kigumu."
Kabla ya msiba huo, msanii huyo aliandika kupitia akaunti yake kuwa Keron yupo katika hali mbaya baada ya kushambuliwa na pumu akiwa shuleni.
Mungu ailaze roho ya Keron mahali pema peponi. AMEN!
 
 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE