July 22, 2014

 
 Taarifa iliyoanza kusambaa usiku wa July 21 ni kuhusu Mabaki ya miili ya watu ambao wanasemekana zaidi ya 100 kukutwa katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji,kata ya Mbweni, wilaya ya Kinondoni,ikiwa imetelekezwa
Taarifa za tukio hilo zilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura ambaye leo atatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.
 
Viungo hivyo vilichukuliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.
Mabaki hayo ya miili yameonekakana kuvuta mamia ya wananchi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo,baadhi ya mashuhuda walipoulizwa wamesema mabaki hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika mifuko ya plastiki ikiwa imefungwa juu.
Wameongeza kwa kusema mabaki hayo ambayo yamekaushwa na kuhifadhiwa katika mifuko ya ujazo wa kilo 25 ni pamoja na miguu, mikono, mbavu na mafuvu ya vichwa hata hivyo Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio na kuanza kupakia mabaki hayo katika gari lao lenye namba za usajili MS 54 UKH na kuipeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Tunaendelea na juhudi za kusikiliza tamko kutoka kwa Jeshi la Polisi juu ya undani wa taarifa hizo
 
Endelea kutembelea blog hii kw ataarifa zaidi

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE