
Norway kujirudishia misaada yake yote nchini kupitia mkataba huu
Zitto Kabwe, Mb
Mkataba
wa mgawanyo wa mapato yanayotokana na uzalishaji wa Gesi Asilia (PSA)
kati ya Shirika la Mafuta Tanzania na Kampuni ya Mafuta ya Norway
umevujishwa (https://onedrive.live.com/view.aspx?cid=0EC42B180C06D0B8&resid=...).Toka
Mkataba huo uvuje na kuanza mijadala kwenye mitandao ya kijamii, habari
zake zimekuwa zinazimwa na hivyo kukosa kabisa mjadala mpana kitaifa na
hasa kwa wananchi wenye rasilimali zao. Mwanzoni wengi wetu tulidhani
(kwa makosa) kuwa tatizo la mkataba huu ni eneo la umiliki wa kampuni tu
(shareholding) kulingana na namna ulivyowasilishwa, kumbe mgawanyo
mzima wa mapato unakwenda kinyume na maelezo ya Serikali na TPDC kwa
umma.
Mkataba
uliovuja unaonyesha kwamba makubaliano ambayo Serikali imeingia na
Wawekezaji hawa kutoka Norway yanaenda kinyume kabisa na mfano wa
mkataba unaotakiwa kusainiwa (Model PSA). Kwa mujibu wa makala
iliyoandikwa na jarida la mtandaoni ( http://africanarguments.org/2014/07/04/leaked-agreement-shows-tanza... )
Tanzania itapoteza zaidi ya shilingi 1.6 trilioni kila mwaka kulingana
na viwango vya uzalishaji wa gesi asilia katika Kitalu namba 2. Kitalu
hiki kinamilikiwa na Kampuni ya StatOil ya Norway na kampuni ya
ExxonMobil ya Marekani. Norway ni nchi inayosifika duniani kwa kupambana
na rushwa na kwa kutumia vizuri rasilimali yake ya mafuta.
Uchambuzi
nilioufanya kulingana na viwango vya mgawo wa mapato kati ya ‘model’
PSA na mkataba huu unaonyesha kwamba Tanzania itapata mgawo kiduchu sana
na kinyume na mgawo unavyopaswa kuwa. Mgawanyo ni
kama ifuatavyo katika majedwali hapa chini; Ikumbukwe kuwa mgawanyo huu
hupatikana baada ya mwekezaji kuondoa gharama zake za uzalishaji,
kinachobakia ndio hugawanywa kati ya mwekezaji na Tanzania.
Jedwali 1 Mkataba wa mgawanyo wa Mapato unaopaswa kutumiwa na TPDC (Model PSA) katika Mikataba na Wawekezaji
Viwango vya uzalishaji kila siku (MMscf per Day)
|
Mgawo wa TPDC (Profit Gas)
|
Mgawo wa Mwekezaji (Profit Gas)
|
|
0
|
249.999
|
50
|
50
|
250
|
499.999
|
55
|
45
|
500
|
749.999
|
60
|
40
|
750
|
999.999
|
65
|
35
|
1000
|
1249.999
|
70
|
30
|
1250
|
1499.999
|
75
|
25
|
1500
|
Above 1500
|
80
|
20
|
Jedwali 2 Mkataba wa mgawanyo wa Mapato kati ya TPDC na Statoil/ExxonMobil.
Viwango vya uzalishaji kila siku (MMscf per Day)
|
Mgawo wa TPDC (Profit Gas)
|
Mgawo wa Mwekezaji (Share of Profit Gas)
|
|
0
|
299.999
|
30
|
70
|
300
|
599.999
|
35
|
65
|
600
|
899.999
|
37.5
|
62.5
|
900
|
119.999
|
40
|
60
|
1200
|
1499.999
|
45
|
55
|
1500
|
Above 1500
|
50
|
50
|
Ukilinganisha
majdwali haya utaona kwamba mgawanyo wa mapato utafaidisha zaidi
kampuni ya StatOil na ni kinyume kabisa na mkataba unavyopaswa kuwa.
Wakati
mgawo wa nusu kwa nusu upo katika uzalishaji wa chini kabisa kwenye
‘model PSA’, kwenye mkataba wa StatOil mgawo huo upo kwenye uzalishaji
wa juu kabisa. Ukilinganisha mgawanyo huu wa mapato, iwapo kiwango cha
‘model PSA’ kingetumika Tanzania ingepata shilingi 1.6 trilioni zaidi ya
kiwango itakachopata kwenye mkataba wa sasa uliovujishwa. Hii ni
kutokana na Bei ambazo Shirika la Fedha la Kimataifa limeweka katika
uchambuzi wake (https://www.imf.org/external/pubs/ft/scr/2014/cr14121.pdf ) kuhusu Gesi asilia ya Tanzania.
Kwa
mujibu wa Mwandishi Ben Taylor katika makala iliyotajwa hapo juu,
kiwango cha mapato ambacho Kampuni ya StatOil ya Norway itajipatia
kutokana na mkataba huu wa kinyonyaji, katika kipindi cha miaka 15 ya
kuzalisha Gesi Asilia nchini itakuwa ni sawa sawa na misaada yote ambayo
Tanzania imepata kutoka Norway toka Tanzania ipate uhuru wake mwaka
1961. Tangu Tanzania ipate Uhuru Norway
imetoa misaada ya thamani ya $2.5 bilioni, wakati kwa mkataba huu na
Kampuni ya StatOil ambayo inamilikiwa na Serikali ya Norway, kwa miaka
15 watapata $5.6 bilioni. Kwa hiyo kwa miaka 7 tu Norway itakuwa
imerudisha misaada yote yake mara mbili zaidi!
Kuvuja
kwa Mkataba huu kumesaidia sana kuona ukweli wa matamko ya viongozi
wetu kuhusu ni namna gani Tanzania itafaidika na utajiri wake wa gesi.
Kama kwa mkataba huu mmoja tu Taifa litapoteza matrilioni ya fedha kiasi
hiki, ipoje hiyo mikataba mingine 29? Hivi sasa ugunduzi wa Gesi Asilia
nchini ni lita za ujazo trilioni 51 ambayo ni sawa na mapipa bilioni 10
ya Mafuta. Katika Gesi Asilia yote iliyopatikana nchini, StatOil peke
yao wana jumla ya lita za uzajo trilioni 20, sawa sawa na mapipa ya
mafuta bilioni 4 (zaidi ya mafuta yaliyogunduliwa nchini Uganda na Ghana
kwa pamoja). Hata hivyo utajiri wote huu utainufaisha zaidi Norway na
Marekani kupitia makampuni yao kuliko watu wa Tanzania. Watanzania
watabakia wanapewa misaada ya vyandarua na mataifa haya ilhali wanafaidi
Gesi Asilia yetu.
Natoa
wito kwa Wizara ya Nishati na Madini kutoa tamko kuhusu mkataba huu
kati ya Shirika la TPDC na StatOil. Vile vile Kampuni hii ya StatOil
kutoka nchi rafiki mkubwa wa Tanzania ina wajibu wa kutoa maelezo ya
kina kuhusiana na mkataba huu. Serikali ieleze ni hatua gani inachukua
kurekebisha Mkataba huu. StatOil nao waeleze watachukua hatua gani
kuhakikisha wanaacha unyonyaji huu mkubwa na wa aibu kwa Taifa la
Norway.
Sasa
ni wakati mwafaka Watanzania kuweza kuona mikataba yote ya Gesi na
Mafuta ambayo Serikali imeingia na Wawekezaji. Uwazi wa Mikataba sasa.
Nimewahi kuandika huko nyuma (PRESS RELEASE: Contracts review is a publicity stunt and creation o...
) kwamba njia pekee ya Watanzania kufaidika na utajiri wa rasilimali
zao ni kuhimiza uwazi wa Mikataba. Mkataba huu wa StatOil uliovujishwa
uwe ni chachu ya kulazimisha Serikali na Makampuni kuweka mikataba yao
wazi. Tuanze mashinikizo haya sasa kwa faida ya vizazi vijavyo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment