July 19, 2014


WANANCHI wa Kigoma Kusini, wamesema wapo tayari kuunganishwa katika kesi ya mbunge wao, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), wakidai kuwa sasa kiburi cha Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inabidi kifike mwisho.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika Kazuramimba, Basanza na Uvinza, wananchi hao walikataa kuuliza maswali mengi badala yake wakitaka kuelekezwa utaratibu ili waweze kuunganishwa kwenye kesi ya mbunge wao.
Mimi sina swali, ninataka kujua ni utaratibu gani unaweza kufanywa ili niweze kuunganishwa katika kesi inayomkabili mbunge wetu, kama mbunge wetu ameitwa tumbili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya CCM ni dharau ya aina gani kwa sisi tuliomchagua, kwanini serikali ya CCM haijamkemea mwanasheria mkuu kutukejeli namna hii?
alisema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Luvakubandi, mkazi wa Basanza.
Pamoja na mkazi huyo kuomba mwongozo huo, wazee kadhaa wa kata za Kazuramimba na Uvinza nao walionekana kukerwa walipofika katika mikutano ya Kafulila.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE