September 15, 2014

DSC_0133

NMB ikiwa ni benki ya chaguo la watanzania wengi,sasa basi taarifa njema ni kwamba (14 Sept) imezindua rasmi kampeni kabambe ‘Weka na Ushinde’ ambayo itakushawishi wewe mteja kuweka fedha benki ili uweze kujipatia ushindi ambao si wa Bajaji,Bodaboda,Baiskeli au fulana za NMB tu bali pia faida kubwa ya riba na usalama wa pesa zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika uzinduzi huo Meneja wa Amana za wateja katika benki hiyo Bw.Boma Raballa amesema kwamba kampeni hiyo itafanyika katika kipindi cha miezi mitatu kuanzi sasa mpaka Desemba 29,2014
Zawadi hizo zinathamani ya zaidi ya TZS 500 Milioni ambazo ni (Bajaji-52,Bodaboda-52,Baiskeli-400 na fulana-500).
DSC_0159 

DSC_0163
Najua mtu wangu wa nguvu utakuwa unajiuliza,Je ni njia ipi sahihi ambayo NMB watatumia kuwapata washindi?- ningependa kukutaarifu kwamba washindi watapatikana kupitia droo ya Bahati Nasibu itakayokuwa ikioneshwa kila siku ya Ijumaa kuanzia saa nne kamili usiku TBC1 na kutangazwa kupitia Magazeti.
Watanzania wote mnaweza kushiriki na nirahisi kwa mteja aliye na akaunti anahitaji kuweka TZS 50,000 kama kiwango cha chini na yule asiye na akaunti anahitaji kufungua akaunti NMB ili aweze kuweka aghalau TZS  50,0.00 kama kiwango cha chini ili aweze kuingizwa kwenye droo ya Bahati Nasibu.
Naye Meneja wa Kanda jijini Dar es Salaam Salie Mlay amesema kwamba zawadi hizo zitatolewa kwenye matawi yote 150 yaliyopo nchini hii ni fursa kwa wananchi kuweza kufaidika na kampeni hiyo.
DSC_0143
Pichani:(Kulia) Meneja wa Amana wateja-NMB Bw.Boma Raballa,Meneja Masoko wa NMB-Rahma Mwapachu,Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam -Salie Mlay
DSC_0175
Zawadi hizo zitakuwa zikikabidhiwa kwa washindi mara moja kwa mwezi kupitia matawi mbalimbali ya NMB yaliyo kwenye kanda husika.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE