October 20, 2014

dmn 
October 18 ilikua ni siku maalum ya Wakazi wa Dar es salaam kula bata kwenye msimu wa mafanikio ambao unapita mara moja kila mwaka kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Ilikua ni good time ya ukweli sana Watanzania kumuona T.I kumuona Davido kumuona Victoria Kimani na Waje pamoja na wasanii wengine wa kimataifa ambao nao walihudhuria tamasha hili lililokuwa na watazamaji zaidi ya elfu hamsini.
Miongoni mwa wasanii waliopokelewa vizuri kwenye show hii ni pamoja na Mr Blue na Micharazo,Ally Kiba,Weusi,Vanessa Mdee,Stamina pamoja na Diamond Platnumz ambaye aliimba single 4 kwenye jukwaa hili.
Mashabiki wengi wa Ally Kiba inasemekana walipanga kuzomea wakati Diamond Platnumz anaperfoam pale jukwaani,kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm meneja wa Diamond Platnumz aitwae Babu Tale kaongelea hali hii.
tale 
Hizi ni sentensi 4 alizozisema.
1.Sisi tumechukulia  sehemu ya mashindano,uzuri sisi tuliambiwa na uongozi wa Clouds kabla ya Diamond hajapanda ilikua saa 3 kamili tukaitwa tukaambiwa kuna watu wamejiandaa kumzomea Diamond.
2.Kama uongozi tulikaa na msanii wetu na kumjenga kisaikolojia na kumwambia kuna hivi vinatokea wao walitaka aanze Davido kisha afate Diamond kupunguza watu watakaozomea tukasema hapana pangeni show yenu kama ilivyokuwa ni sehemu ya mashabiki kufurahi.
3.Hatujaathirika kwamba msanii wetu ameshuka tunapoona watu wanapiga kelele kwa ajili yako au huna sifa ile unatakiwa uangalie umekosea wapi unaenda wapi,hatuna makosa kwa mashabiki wetu.
4.Kikubwa Diamond anafanya vizuri tunatakiwa kuhamisha macho yetu tumpigie kura Diamond kwenye tuzo za Channel  O Music Awards, kwa sababu mwisho wa siku chema chajiuza kibaya chajitembeza.

Related Posts:

  • Gari la kikosi cha Zimamoto limevunjwa vioo   Picha hii siyo halisi ya tukio   Jeshi la Polisi mjini Tunduma mkoani Mbeya limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya vijana waliofunga barabara. Akiongea na East Africa Radio kwa njia ya simu Kaman… Read More
  • Makamu wa rais wa afutwa kazi    Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amemfuta kazi makamu wa rais kwa kutafuta hifadhi katika ubalozi wa kigeni nchini humo.Siku ya jumamosi ,Samuel Sam Sumana amesema kuwa alimtaka balozi wa Marekani kump… Read More
  • Fid Q, K-sha wapata tuzo zaheshima za EU    Kutoka kulia ni baadhi ya Watanzania waliotunukiwa Tuzo ya Heshima na Umoja wa Ulaya nchini EU, kutokana na mchango wao katika kuliletea taifa maendeleo.   Umoja wa Ulaya nchini umewatunuku tuzo za hes… Read More
  • Makinda: Zitto Kabwe ni mbunge halali   Spika wa Bunge Mh Anne Makinda amesema kuwa kwa niaba ya Bunge bado anamtambua mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuwa ni mbunge halali wa bunge hilo. Akizungumza nje ya ukumbi wa bunge mara baada ya kikao… Read More
  • Umeipata hii ya majaji 3 kufutwa kazi kwa kutazama video za ngonoMajaji watatu wamefutwMajaji watatu wamefutwa kazi kwa kutumia muda wao afisini kutizama filamu za ngono. Jaji Timothy Bowles anayesikiza kesi za wilaya , jaji wa maswala ya uhamiaji Warren Grant na jaji Peter Bullock wamefut… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE