October 29, 2014

Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo akizindua tawi jipya la timu hiyo leo. (Picha na Yanga SC)
UONGOZI wa Klabu ya Young Africans uliopo na timu mjini Kahama, leo umefungua tawi la wanachama lenye jumla ya wanachama mia tatu (300) na kuhudhuriwa na wapenzi, washabiki na wadau lukuki.
Mkuu wa msafara, Mohamed Bhinda alimkaribisha kocha mkuu wa timu hiyo, Marcio Maximo kuzindua tawi hilo mara baada ya mazoezi ya asubuhi akiwa ameambatana na benchi la ufundi na wachezaji wa timu ya Young Africans.
Mara baada ya uzinduzi wa tawi hilo wapenzi, washabiki na wanachama walipata fursa ya kuongea na kupiga picha na wachezaji wa Young Africans, benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi walioambatana na timu.
Jioni ya leo majira ya saa 10:00 jioni Young Africans itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji timu ya Ambassador FC katika Uwanja wa Taifa mjini Kahama kabla ya kuanza safari ya kuelekea mjini Bukoba.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE