January 28, 2015

 
 CLUB Olympia iliyoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam, imeungua na kuteketea kwa moto majira ya saa kumi na nusu usiku wa kuamkia leo ambapo chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika mapema.
Mlinzi wa club hiyo inayomilikiwa na Samuel Mwaisumbe, na ambaye hakuweza kujitambulisha jina lake, alisema moto huo ulianza mishale ya saa kumi usiku ambapo waliweza kutoa taarifa kwa vyombo vya zima moto.

  
Aliongeza kwamba zima moto hawakufika kwa muda mwafaka na badala yake walifika kunako saa 12 asubuhi wakiwa na maji kidogo ambayo yaliisha wakati moto ukiendelea.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE