Ofisi kuu ya Chama cha wananchi CUF
KUFUATIA
kuibuka kwa fujo na adha mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za
mitaa nchini, kuanzia zoezi la upigwaji wa kura mpaka uapishwaji wa
wenyeviti hao kuzua utata, Chama cha Wananchi (CUF) leo kimewataka
Waziri wa Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia
na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kinondoni na kujiuzulu kwa vile wameshindwa
kuendesha uchaguzi huo.
Aidha Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Tanzania Bara, Magdalena Sakaya,
ametaja baadhi ya maeneo yaliyogubikwa na fujo hizo katika uapishwaji wa
wenyeviti kuwa ni pamoja na Kawe, Kinondoni, Mwananyamala, Kiwalani,
Buguruni, Kinyerezi, Migoba, Kigogo na kwingineko.
Je, unakubaliana na lawama hizo kupelekwa TAMISEMI?
0 MAONI YAKO:
Post a Comment