Mwanamuziki Ray C ambae alitamba miaka ya nyuma na ngoma kali kibao
ikiwemo Na wewe milele,Sogea sogea na nyingine nyingi amefunguka na
kusema kuwa kwa sasa hakuna mtu atakae weza kutembelea nyota yake katika
muziki kwani sasa maisha yake
ameyakabidhi
kwa Mwenyezi Mungu ambaye ndiye mlinzi wake na mwongozaji wake katika
maisha,Ray C amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instragram.
"Tatizo Nyota.........Kwa sasa ameishikilia Mola wangu pekee hakuna atakaeitembelea tena! !!!!!!!!MSHUMMSHUM"
Mwanamuziki Ray C ambae alikuwa kimya kwa muda mrefu katika tasnia ya
muziki alipatwa na matatizo ya utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo kwa
namna moja au nyingine ndiyo yalifanya awezekupotea katika tasnia hata
kuchangia pia kwa baadhi ya mambo yake ya maendeleo kushindwa songa
lakini baadae mwanamuziki huyo aliweza kutoka katika mtego huo kwa
kuacha kabisa kutumia madawa ya kulevya na kuwa mwanaharakati tena
mstari wa mbele kuwaokoa wasaniii wengine ambao nao walitumbukia katika
matumizi ya dawa za kulevya.
Ray C ameweka wazi kuwa katika kipindi ambacho yeye alikuwa na
matatizo kuna kundi la watu au baadhi ya watu walikuwa wanafurahia na
hawakupenda kwa mwanamuziki huyo kumwona anachomoka katika matatizo
ambayo yalikuwa yanamsonga yakiwemo ya matumizi ya dawa za kulevya na
pia hawakupenda kuona mwanamuziki huyo anarudi katika muziki kama
ilivyokuwa awali,bali walitamani hata angekufa kwa matumizi ya dawa za
kulevya,haya yote amefunguka leo.
"Nakuona wewe hapo,najua unanichukia na unatamani ningefia mbali na
uteja!Unatamani nisingepona! Unatamani nisingerudi kwenye muziki wewe
apo! Pole mwaya Mungu hajapenda niondoke so talk to my....... coz my
face doesn't wanna see u"
Katika siku za hivi karibuni Ray C amekuwa katika mkakati kabambe wa
kupunguza mwili wake ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida
ambayo zamani ilikuwa ikiwashika watu na kufanya watu kumpatia jina la
kiuno bila mfupa kutokana na uwezo wake stejini na kuweza kucheza na
mwili wake.
Ray C ni miongoni mwa wasanii wa zamani katika game ya bongo fleva
ambao bado wana nia na hamu ya kuona wanarudi katika muziki na
kushindana na soko la muziki wa sasa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment