January 08, 2015

 
  Leo jioni, Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na Golikipa wake Juma Kaseja kuanzia leo baada ya kuwepo kwa hali ya kutoelewana baina ya kipa huyo na uongozi wa klabu.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro amethibitisha taarifa hizo na kusema kuwa Juma Kaseja alivunja masharti ya mkataba huo kwa kutohudhuria mazoezini na kuongeza kuwa Juma mwenyewe alishaonesha nia ya kuondoka klabuni hapo hivyo ni bora klabu hiyo ikamuachia.
Muro amesema “Yanga haijavunja mkataba na Kaseja bali imemuachia baada ya Kaseja mwenyewe kuvunja masharti ya mkataba kati yake na Yanga...”

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE