Watu wenye silaha wameshambulia
hoteli moja maarufu kufikiwa na wageni kutoka nje katika mji mkuu wa
Libya, Tripoli, na kuua walinzi watatu na watu wengine 12 kujeruhiwa.
Watu
kadha wenye silaha walivamia hoteli ya Corinthia mjini Tripoli na
kufyatua risasi katika eneo la mapokezi. Bomu lililokuwa limetegwa
katika gari lililipuka nje ya hoteli.
Baadhi ya watu wenye silaha bado wanasadikika kuwa wako ndani ya
hoteli. Haifahamiki kama wafanyakazi au wageni wangali katika hoteli
hiyo.
Mgeni mmoja raia wa Ufilipino, alikuwa miongoni mwa majeruhi wa tukio hilo.
Akaunti
moja ya mtandao wa twitter inayohusishwa na na kikundi cha Islamic
State imesema kundi hilo limeshambulia hoteli hiyo. Madai hayo
hayajathibitishwa.
Raia mmoja waliyeshuhudia
shambulio hilo ameiambia BBC: "ghafla nilisikia milio ya risasi na kuona
watu wakikimbia kuja upande wangu, na wote tulitoroka kupitia nyuma ya
hoteli kupitia njia ya chini ya gereji."
Jumla ya washambuliaji haifahamiki. Vyanzo mbalimbali katika eneo la
tukio vinasema kulikuwa na washambuliaji kati ya watatu na watano.
Habari
za ulama zimeiambia BBC kuwa mtu mmoja mwenye silaha amekamatwa na
washambuliaji wengine wawili bado wako ndani ya hoteli.
Majeshi ya
usalama yamekusanyika kuzunguka hoteli kufuatia mlipuko na eneo kuzunguka hoteli hiyo
limefungwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment