January 29, 2015


TAREHE 26-27 JANUARY YA KILA MWAKA CHAMA CHETU KIMEJIWEKEA UTARATIBU WA KUFANYA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MATUKIO YA UDHALILISHAJI, UNYANYASAJI NA MAUAJI YALIYOFANYWA NA JESHI LA POLISI NCHINI MWEZI JANUARY MWAKA 2001 BAADA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2000. MAADHIMISHO HAYA YANALENGO LA KUWAENZI WATANZANIA WENZETU WALIOJITOA MUHANGA KUDAI KATIBA MPYA YENYE MISINGI YA DEMOKRASIA YA KWELI NA INAYOKIDHI MFUMO WA VYAMA VINGI VYA SIASA NCHINI, TUME HURU YA UCHAGUZI NA KUWEPO KWA DAFTARI SAHIHI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA SAMBAMBA NA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MWAKA 2000 ZANZIBAR AMBAO TUME ILISHIRIKI KUFANYA UCHAFUZI WA MATOKEO HAYO.
WANANCHI WALIANDAMANA NA KUDAI KUREJEWA KWA UCHAGUZI HUO NA KUPELEKEA MATUMIIZI MAKUBWA YA JESHI LA POLISI YASABABISHA KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA NCHI YETU KUWEPO KWA WAKIMBIZI WA KISIASA KATIKA NCHI YETU.
JUZI TAREHE 27 JANUARY, 2015 CHAMA CHETU CHA CUF KILIPANGA KUFANYIKA MAANDAMANO NA BAADAE MKUTANO WA HADHARA KATIKA VIWANJA VYA ZAKHEEM,MBAGALA-DSM, BAADA YA KUTOA TAARIFA KWA VOMBO HUSIKA TAREHE 22/01/2015 WIKI MOJA KABLA.
CHAKUSIKITISHA TAREHE 26 JIONI JESHI LA POLISI LILITOA TAARIFA YA KUSITISHA MAANDAMANO HAYO NA MKUTANO WA HADHARA KWA MADAI YA SABABU ZA KIINTELIJENSIA.
MBALI NA MWENYEKITI WA TAIFA KUKUBALIANA NA SABABU HIZO ZISIZO NA UKWELI UNAOJITOSHELEZA ALIAHIRISHA MAANDAMANO HAYO NA KUWAOMBA WAFUASI KUREJEA MAJUMBANI KWA AMANI. KWA KUWA MAANDAMANO YALIKUWA YAANZIE OFISI YA CUF WILAYA YA TEMEKE NA KUISHIA VIWANJA VYA ZAKHEEM KWA MKUTANO WA HADHARA, ILILAZIMIKA KUONDOKA KWA KUTUMIA MAGARI KWENDA VIWANJA VYA ZAKHEEM KUAHIRISHA MKUTANO HUO AMBAPO KULIKUWA NA WANANCHI WENGI WAKISUBIRI KUMSIKILIZA MWENYEKITI WETU TAIFA PROFESA IBRAHIM LIPUMBA.
HATA HIVYO, JESHI LA POLISI HALIKUKUBALIANA NA HAYO NA KUZUIA NJIA PALE TEMEKE HOSPITALI, BAADA YA MVUTANO MKUBWA NA JESHI LA POLISI PALE BARABARANI LIKIWA LIMETANDA NA KUZUIA MSAFARA WA GARI LA MWENYEKITI TAIFA KUTOKWENDA MBAGALA, NA KUWASHINDA KWA HOJA WAKARUHUSU KUPITA ENEO HILO. LAKINI WALIDAI KUWA WAO WANAPOKEA ‘ORDER’ KUTOKA JUU. GHAFLA WAKAUFUATA MSAFARA HUO NA KUUZUIA TENA ENEO LA MTONI MTONGANI NA KUZIBA BARABARA, KUPIGA MABOMU YA MACHOZI HOVYO, KUPIGA WATU NA KUATHIRI SHUGHULI MBALIMBALI ZA WANANCHI WA ENEO HILO, KUMKAMATA PROFESA LIPUMBA NA WALINZI WAKE, VIONGOZI NA WAFUASI WENGINE WA CHAMA CHETU.
• CUF – CHAMA CHA WANANCHI TUNALAANI KITENDO HICHO CHA JESHI LA POLISI NCHINI KUTUMIKA KISIASA KUZUIA SHUGULI HALALI ZA VYAMA VYA UPINZANI NCHINI NA KUWARUHUSU CCM KUFANYA WANAYOTAKA BILA KUBUGHUDHIWA NA VYOMBO VYA DOLA WALA VISINGIZIO VYA SABABU ZA KIINTELIJENSIA.
• TUNALAANI KUMKAMATA MWENYEKITI WETU WA TAIFA, KUMDHALILISHA PASINA KUWEPO KWA MAANDAMANO AMBAYO CUF NA VIONGOZI WAKE WALISHAKUBALIANA KUTOYAFANYA.
• TUNALAANI KUPIGWA KWA VIONGOZI NA WAFUASI WA CHAMA CHETU NA JESHI LA POLISI, NA TUNALITAKA JESHI LA POLISI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA KUTUMIA WELEDI NA KUACHA USHABIKI NA KUTUMIWA KISIASA KWAVISINGIZIO VYA KIINTELIJENSIA. VINGINEVYO JESHI LITAIINGIZA NCHI YETU KATIKA GHASIA NA VURUGU AMBAZO ATHARI YAKE HAITAKUWA YA UPANDE MMOJA PEKEE.
• IWEJE PEMBA AMBAPO KUNA WAATHIRKA WAKUBWA WA MATUKIO YA MAUAJI HAYO, UDHALILISHAJI NA UONEVU WA KADHIA HII, WAKIWEPO WAJANE NA MAYATIMA WENGI IRUHUSIKE KUFANYIKA MKUTANO NA WALA HAKUKUWA NA SABABU ZA KIINTELIJENSIA LAKINI ZAKHEEM, MBAGALA- DAR ES SALAAM IZUILIWE? NDO KUSEMA KUWA HUU NI UKADA WA JESHI LA POLISI BARA (TANGANYIKA)?
• IWEJE JESHI LA POLISI LISIWE NA NGUVU YA KULINDA USALAMA WAKATI WA MAANDAMANO NA MKUTANO WA HADHARA, LAKINI LINAKUWA NA NGUVU KUBWA YA KUPIGA RAIA WASIO SILAHA, KUWAKAMATA, NA KUHARIBU SHUGHULI ZA WANANCHI HUKU WAKIJIHUSISHA NA VITENDO VYA KUPORA SIMU NA FEDHA ZA WATUHUMIWA?
• TUKIWA TUNAELEKEA MWEZI OKTOBA KATIKA UCHAGUZI MKUU, TUNAMTAKA MHE RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE, KUZUNGUMZA NA WATENDAJI WA SERIKALI YAKE ILI KUIVUSHA NCHI YETU SALAMA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MAJANGA YA UFISADI WA TEGETA ESCROW, VITA VYA URAIS MIONGONI MWAO WANACCM, KATIBA PENDEKEZWA INAYOKATALIWA NA WATANZANIA.
• TUNAMTAKA MHESHIMIWA RAIS AWEKE MAZINGIRA SAWA YA USHINDANI WA KISIASA NCHINI KUELEKEA OKTOBA, ILI KUJENGA MUSTAKBALI MWEMA WA TAIFA LETU, OMBWE LA UONGOZI LISIJE LIKAIINGIZA NCHI KATIKA MAPIGANO YA WENYEWE KWA WENYEWE AMBAYO MADHARA YAKE HAYATAKUWA YA UPANDE MMOJA.
• CUF CHAMA CHA WANANCHI TUNAWEKA WAZI MSIMAMO WETU KUWA, KILA TAREHE 27 JANUARY YA KILA MWAKA TUTAENDELEA KUFANYA MAANDAMNO NA MIKUTANO YA HADHARA MAENEO MBALIMBALI NCHINI IKIWA NI SEHEMU YA KUWAENZI NA KUWAKUMBUKA NDUGU ZETU WALIOJITOLA MUHANGA KWA UKOMBOZI WA KIDEMOKRASIA KATIKA NCHI YAO.
• JESHI LA POLISI KAMA HAWATAKI KUELEWA HILO WAKAE MKAO WA MAPAMBANO NA WANANCHI WATANZANIA KILA MWAKA NA NADHANI MAADHIMISHO YA MWAKA 2016 JANUARY YATAKUWA MAKUBWA ZAIDI KWA KULINGANA NA JESHI LA POLISI LITAKAVYOKABILIANA NAYO.
• JESHI LA POLISI WALIPASWA WAPIGANE DHIDI YA WEZI NA MAFISADI WA FEDHA ZA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW ULIOFANYWA NA WAKUBWA WA SERIKLI YA CCM.
• HATA HIVYO HATUSHANGAI KWA SERIKALI YA CCM PAMOJA NA MAFISADI KUTAJWA WAZI BUNGENI NA KWA USHAHIDI LAKINI HAKUNA ALIOWAJIBISHWA. NGUVU ZAO NI DHIDI YA WATETEZI WA WATANZANIA.
• POLISI WAMEZOEA KUUA, TUNA MIFANO MINGI YA KUDHIBITISHA TABIA HII. GESI YA MTWARA, MWANGOSYA, MKUTANO WA DONGE MAHONDA ZANZIBAR, ARUSHA ,MOROGORO, SHEKH PONDA KUPIGWAA RISASI, NAKADHALIKA.
• JESHI LA POLISI LIMEKOSA MAADILI HALIFAHI, LINAHITAJI MAREKEBISHO MAKUBWA NA TUNAMTAKA MHE RAIS KUWAWAJIBISHA WAHUSIKA WOTE WA TUKIO HILI –VIONGOZI WA JESHI LA POLISI.
• SERIKALI YA CCM INAPASWA KUJIFUNZA KUTOKA NCHI ZINGINE, UWEZI KUHUBIRI AMANI HUKU UNAANZISHA NA KUSABABISHA MATUKIO YA UVUNJWAJI WA AMANI. KWA KAWAIDA MNYONGE HUWA HAFANYI FUJO BALI HUJITETEA.
• TUNAWAPONGEZA WABUNGE WETU WOTE NA TIMU YA UKAWA KWA KUWA PAMOJA KATIKA KADHIA HII YA MUENDELEZO WA UONOVU UNAOFANYWA NA JESHI LA POLISI KWA KUITAKA SERIKALI ITOE MAELEZO NDANI YA BUNGE NA KUJADILIWA.
• TUNAVISHUKURU VYOMBO VYA HABARI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI YA MABOMU KUWEZA KULILIPOTI SUALA HILI KWA UKAMILIFU WAKE NA KWA USAHIHI.
• THE CIVIC UNITED FRONT(CUF-CHAMA CHA WANANCHI) PAMOJA NA WASHIRIKA WENZETU WA UKAWA TUTAENDELEA KUWA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA KUWA HAKI, AMANI, DEMOKRASIA NA MAENDELEO KWA WATANZANIA WOTE YANAPATIKANA NCHINI, TUTENDELEA KUPIA VITA NA KUPINGA UFISADI WA MALI ZA UMMA NA UFISADI WA MATUMIZI MABAYA YA MAMLAKA KAMA YANAVYOTUMIWA NA JESHILA POLISI.
• CUF NA UKAWA TUNAWAOMBA WATANZANIA WOTE WAPENDA HAKI NA MAENDELEO YA NCHI YAO KUUNGA MKONO JUHUDI HIZI ZA KUUONDOA UTAWALA WA DHULMA, UONEVU, UFISADI UNAOFANYWA NA SERIKALI YA CCM NA VYOMBO VYAKE.
HAKI SAWA KWA WOTE

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE